• HABARI MPYA

    Monday, July 04, 2016

    KIPA ‘NGONGOTI’ MSPANYOLA ATUA AZAM FC

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIPA Juan Jesus Gonzalez (pichani kushoto) amewasili leo nchini kutoka Hispania kujaribu kujiunga na mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC.
    Kipa huyo amepokewa na Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Iddi Maganga leo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam tayari kwa majaribio.
    Katika hatua nyingine, jopo la makocha sita kutoka liliwasili juzi Dar es Salaam kuanza maandalizi ya msimu ujao wa 2016-2017).
    Hao ni Kocha Mkuu Zeben Hernandez, Msaidizi wake Yeray Romero, Kocha Mkuu wa Viungo Jonas Garcia, Msaidizi wake, Pablo Borges na kocha wa Makipa Jose Garcia.
    Jopo hilo la makocha litaongezewa nguvu na makocha wengine wazawa waliokuwa na Azam FC msimu uliopita, Kocha Msaidizi Dennis Kitambi na wa Makipa, Idd Abubakar.
    Aidha, Daktari mpya wa timu hiyo, Sergio Perez, anatarajia kutua nchini Julai 12 mwaka huu kutoka Hispania pia
    Makocha hao wanatua nchini kuziba nafasi za benchi la ufundi lililopita la Azam FC chini ya Stewart Hall, Msaidizi wake Mario Marinica na Mtaalamu wa Viungo, Adrian Dobre, waliojiuzulu kuinoa timu hiyo mara baada ya mchezo dhidi ya JKT Ruvu (2-2) msimu uliopita.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIPA ‘NGONGOTI’ MSPANYOLA ATUA AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top