• HABARI MPYA

  Saturday, July 02, 2016

  SERENGETI BOYS WASONGA MBELE, WAWATANDIKA 6-0 SHELISHELI KWAO

  Na Alfred Lucas, VICTORIA
  TIMU ya taifa ya vijana ya Tanzaia chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imeshinda mabao 6-0 dhidi ya Shelisheli katika mchezo wa marudiano Raundi ya Kwanza kufuzu Fainali za U17 Afrika mwakani Madagascar jioni ya leo Uwanja wa Stade Linite mjini Victoria. 
  Kwa matokeo hayo, Serengeti Boys inasonga mbele Raundi ya Pili na hatua ya mwisho ya mchujo kwa ushindi wa jumla wa 9-0 baada ya wiki iliyopita kushinda 3-0 katika wa kwanza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Serengeti Boys sasa itamenyana na Afrika Kusini, hayo yakiwa ni marudio ya mchezo wa mwaka jana katika hatua hiyo hiyo, ambayo vijana wa Tanzania walitolewa.
  Serengeti Boys imesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 9-0
  Mabao ya Serengeti leo yamefungwa na Shaaban Zubeiry dakika ya sana, Mohammed Abdalah dakika ya 49, Hassan Juma mawili dakika ya 47 na 75, Issa Makamba kwa penalti dakika ya 65 na Yohana Nkomola dakika ya 90.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERENGETI BOYS WASONGA MBELE, WAWATANDIKA 6-0 SHELISHELI KWAO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top