• HABARI MPYA

  Wednesday, July 06, 2016

  SIMBA WAENDA MOROGORO KUWEKA KAMBI, WAKIRUDI WANAKIPIGA NA GOR MAHIA SIMBA DAY

  Na Somoe Ng'itu, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC inatarajiwa kuondoka mjini Dar es Salaam keshokutwa kwenda Morogoro kuweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ambao utanatarajiwa kuanza kuanzia Agosti 20, mwaka huu.
  Na baada ya maandalizi mazuri ya takriban mwezi mzima, Simba imeialika klabu bingwa ya Kenya, Gor Mahia kwa ajili ya kuja nchini kucheza mechi ya kirafiki katika Tamasha la Simba Day, Agosti 8.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE jana, Rais wa Simba, Evans Elieza Aveva alisema kwamba uongozi wa timu hiyo uliamua kuahirisha programu ya mazoezi iliyopangwa kuanza jana mjini Dar es Salaam kwa ajili ya kupisha sherehe za Sikukuu ya Eid El Fitri.
  Rais wa Simba, Evans Aveva akimkabidhi jezi kocha Omog wiki iliyopita baada ya kusaini Mkataba wa miaka miwili
  Meneja huyo wa zamani wa Embassy Hotel, Aveva alisema kuwa wachezaji wote waliosajiliwa na timu hiyo watakwenda kambini Morogoro kwa ajili ya kuanza kujifua wakiwa chini ya Kocha Mkuu mpya Mcameroon Joseph Marius Omog ambaye aliwasili nchini wiki iliyopita na kurithi mikoba ya Muingereza Dylan Kerr, aliyefukuzwa Januari.
  "Kila kitu kinakwenda vizuri na Mungu akijaalia baada ya sikukuu kupita, timu itakwenda Morogoro na si Lushoto kama ilivyoandikwa na gazeti moja," alisema Aveva.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA WAENDA MOROGORO KUWEKA KAMBI, WAKIRUDI WANAKIPIGA NA GOR MAHIA SIMBA DAY Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top