• HABARI MPYA

  Saturday, July 02, 2016

  MAUMIVU YA MAZEMBE BADO YAMTESA MAHADHI WA YANGA

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  KIUNGO mpya wa Yanga, Juma Mahadhi leo ameshindwa kuendelea na mazoezi baada ya kujitonesha nyonga aliyoumia katika mchezo dhidi ya TP Mazembe Jumanne.
  Yanga ilifungwa 1-0 na TP Mazembe ya DRC katika mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika Jumanne Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na siku hiyo Mahadhi kwa mara ya kwanza alianzishwa baada ya kusajiliwa mwezi uliopita kutoka Coastal Union ya Tanga.
  Hata hivyo, kiungo huyo chipukizi alidumu uwanjani kwa dakika 69 tu kabla ya kuumia na kumpisha Geoffrey Mwashiuya.
  Juma Mahadhi ameshindwa kufanya mazoezi Yanga leo kutokana na maumivu

  Mahadhi alijaribu kurudi uwanjani leo, Boko Veterani, lakini akashindwa kuendelea baada ya kujinotesha nyama.
  “Nimejaribu kufanya mazoezi, lakini nimeumia, yaani nimejitonesha kwa hivyo ninajisikia maumivu na nimeshindwa kuendelea,”alisema.
  Haijulikani maumivu haya ya Mahadhi yatachukua muda gani, kwani klabu yake inakabiliwa na mchezo mwingine wiki mbili zijazo.
  Baada ya kupoteza mechi zote mbili mfululizo za mwanzo za Kundi A, ikifungwa 1-0 na MO Bejaia nchini Algeria na 1-0 na Mazembe Jumanne, Yanga itashuka tena dimbani Julai 17 kumenyana na Medeama ya Ghana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Na ikumbukwe Yanga ndiyo inashika mkia katika Kundi A, ikiwa haina pointi wakati Mazembe, yenye pointi sita inaongoza ikifuatiwa na MO Bejaia yenye pointi nne na Medeama pointi moja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAUMIVU YA MAZEMBE BADO YAMTESA MAHADHI WA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top