• HABARI MPYA

  Friday, July 08, 2016

  SAMATTA TENA, AFUNGA KRC GENK IKIUA 4-0 MCHEZO WA KIRAFIKI

  Na Mwandishi Wetu, GENK
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ameendelea kung'ara katika klabu yake, KRC Genk ya Ubelgiji baada ya jana kufunga bao moja katika ushindi wa 4-0 ugenini dhidi ya Lommel United.
  Nahodha huyo wa Tanzania, Taifa Stars jana alifunga dakika ya 46 bao la tatu katika mchezo huo wa kirafiki, baada ya Kumordzi kutangulia kufunga la kwanza dakika ya 33 na Bailey la pili dakika ya 35.
  Aliyehitimisha karamu ya mabao ya KRC Genk inayojiandaa na mechi za mchujo za Europa League alikuwa ni Trossard aliyefunga bao la nne dakika ya 68.
  Kikosi cha KRC Genk jana kilikuwa; Bizot, Walsh/Castagne dk83) Dewaest, Kumordzi, Uronen, Ndidi, Pozuelo/Sabak dk77), Bailey/Trossard dk45, Buffalo/Karelis dk72, Samatta/de Camargo dk72) na Kebano/Tshimanga dk77.
  Wiki iliyopita Samatta alifunga mabao mawili mfululizo ndani ya siku mbili katika mechi za kirafiki pia.
  Mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba SC, alifunga bao moja katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Bocholt Julai 1 na akafunga tena bao moja katika ushindi wa 3-0 Julai 2 dhidi ya ESK Leopoldsburg.
  Mbwana Samatta ameendeleza moto wa mabao KRC Genk baada ya ja a kufunga katika ushindi wa 4-0

  VIDEO; SAMATTA ALIVYOFUNGA JANA KRC GENK IKIUA 4-0


  Kabla ya mechi hiyo ya Julai 1, Samatta aliichezea pia Genk katika mchezo wa kirafiki Juni 25, ikishinda 7-1 dhidi ya Unity Termien.
  Lakini siku hiyo, Samatta hakufunga na mabao ya timu yake yalifungwa na de Camargo, Dewaest, Kebano, Sabak, Van Zeir, Karelis na Pozuelo huku la wapinzani wao likifungwa na Baur.  
  Genk watashuka tena dimbani Julai 9 kumenyana na Lierse na Julai 17 na FC Eindhoven.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA TENA, AFUNGA KRC GENK IKIUA 4-0 MCHEZO WA KIRAFIKI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top