• HABARI MPYA

  Friday, July 01, 2016

  RASMI, IBRAHIMOVIC NI MCHEZAJI MPYA WA MAN UNITED

  MSHAMBULIAJI Zlatan Ibrahimovic hatimaye amethibitisha anakwedna Manchester United msimu ujao.
  Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 34 safari yake ya kwenda kuungana na kocha Jose Mourinho imekuwa moja ya siri zilizotunzwa vizuri katika soka.
  Hata hivyo, Ibrahimovic ameamua kuthibitisha hilo Alhamisi kupitia ukurasa wake wa Instagram soka moja nyuma kabla ya ilivyotarajiwa.
  Zlatan bado hajasaini Mkataba Man United wala kufanyiwa vipimo vya afya, lakini wamefurahia mchezaji huyo kutangaza habari hizo.
  Namna ambavyo Zlatab Ibrahimovic ataonekana katika jezi ya Manchester United msimu ujao  PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  WASIFU WA ZLATAN IBRAHIMOVIC: 

  Kuzaliwa: Oktoba 3, 1981 (Miaka 34)
  1999-01 Malmo – Mechi 47 mabao 18
  2001-04 Ajax – Mechi 110 mabao 48
  2004-06 Juventus – Mechi 92 mabao 26
  2006-09 Inter Milan – Mechi 117 mabao 66
  2009-10 Barcelona – Mechi 46 mabao 22
  2010-12 AC Milan – Mechi 85 mabao 56
  2012-16 PSG – Mechi 180 mabao 156
  2001-16 Sweden – Mechi 116 mabao 62
  TOTAL: Jumla Mechi 793 mabao 454
  Mataji: Eredivisie (2002, 2004), Kombe la KNVB (2002), Serie A (2007, 2008, 2009, 2011), Super Cup ya Italia (2006, 2008, 2011), La Liga (2010), Super Cup ya Hispania (2009, 2010), Super Cup ya UEFA (2009), Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA (2009), Ligue 1 (2013, 2014, 2015, 2016), Coupe de France (2015, 2016), Coupe de la Ligue (2014, 2015, 2016), Trophee des Champions (2013, 2014, 2015)
  Mshambuliaji huyo wa Sweden anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya Ijumaa baada ya kufikia makubaliano ya Mkataba na United wiki kadhaa zilizopita kwamba atalipwa Pauni 200,000 kwa wiki.
  Ibrahimovic ameposti picha ya nembo ya Manchester United akiambatanisha na maelezo yasemano: "Wakati wa kuifahamisha dunia,". Alimalizia katika maelezo yake chini ya picha kwa kuandika '#ninakuja'.
  Nyota huyo wa zamani wa Barcelona na Inter Milan, alikataa kuongeza Mkataba katika klabu yake, Paris Saint-Germain na mapema ilifahamika atakwenda kuungana na Mourinho aliyechukua nafasi ya Louis van Gaal Uwanja wa Old Trafford. 
  Atasaini rasmi Mkataba Ijumaa na kuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Mourinho’ tangu atambulishwe kuwa kocha mpya wa United.
  Mourinho wakati wote alipenda kuungana tena na Ibrahimovic aliyewahi kufanya naye kazi kwa mafanikio walipokuwa Inter Milan ya Italia. 
  Baada ya kumalizana na Ibrahimovic, United imeingia rasmi kwenye majadiliano na Juventus ya Italia juu ya kiungo kumsajili tena kiungo wake wa zamani, Mfaransa Paul Pogba.
  Kwa mujibu wa gazeti la L'Equipe la Ufaransa, Pogba, mwenye umri wa miaka 23 sasa, aliyeondoka Man United kuhamia Juventus kama mchezaji huru mwaka 2012 baada ya kukataa kuongeza Mkataba chini ya kocha Sir Alex Ferguson kutokana na kutopewa nafasi ya kucheza, sasa anaweza kurejea Old Trafford.
  Chini ya Ferguson, Pogba alicheza mechi saba tu za kikosi cha kwanza Man United, lakini sasa chini ya kocha Mreno, Jose Mourinho Mashetano hao Wekundu wanataka kumrejesha Old Trafford.
  Na inasemekana Juve, maarufu kama Kibibi Kizee cha Turin haiwezi kumuuza nyota wake huyo kwa dau la chini ya Pauni Milioni 82.8..
  L'Equipe limesema kwamba , kocha mpya wa Man United, Jose Mourinho anataka kutambulisha mfumo wa 4-3-3 msimu ujao na anamtaka Pogba akachezea pamoja na Nahodha Wayne Rooney katika safu ya kiungo katikati, pamoja na mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic, Anthony Martial na Henrikh Mkhitaryan pembeni.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RASMI, IBRAHIMOVIC NI MCHEZAJI MPYA WA MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top