• HABARI MPYA

  Tuesday, July 05, 2016

  KOCHA GHALI ZAIDI AFRIKA 'ATUPIWA VIRAGO' VYAKE GABON

  WENYEJI wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani, Gabon wamemfukuza kocha wao Jorge Costa ikiwa ni miezi sita kabla ya kuanza kwa michuano hiyo Januari.
  Kocha huyo Mreno aliajiriwa Julai 2014, na amefukuzwa mara tu baada ya kupangwa droo ya kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2018, Gabon ikiwekwa kundi moja na Ivory Coast, Mali na Morocco.
  Costa alikuwa ndiye kocha anayelipwa zaidi kuliko wengine wote wanaofanya kazi bara hiili kwa mujibu wa taarifa za tovuti ya Gaboneco mwezi Mei.
  Kocha ghali zaidi barani Afrika, Jorge Costa amefukuzwa kazi Gabon ikiwa ni miezi sita kabla ya Fainali za Mataifa ya Afrika

  "Kama ninapokea Euro 70,000 kwa mwezi, mshahara ambao unaonifanya niwe kocha anayelipwa vizuri zaidi Afrika, ni kwa sababu mimi ni kocha bora," alisema kocha na mchezaji huyo wa zamani wa Porto na Standard Liege, Costa.
  Alitoa maelezo hayo baada ya maswali kuanza kuibuka juu ya kiwango cha Gabon uwanjani, hususan wakifungwa 2-1 na mabingwa wa Afrika, Ivory Coast katika mchezo wa kirafiki hivi karibuni.
  Gabon, waliokuwa wenyeji washirika wa Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2012 pamoja na Equatorial Guinea, watakuwa wenyeji wa fainali za 2017 kuanzia Januari 21 hadi Februari 12.
  Mrithi wa Costa anatarajiwa kutajwa Julai 30 tayari kwa mchezo wa kwanza wa kufuzu Kombe la Dunia mwezi Oktoba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOCHA GHALI ZAIDI AFRIKA 'ATUPIWA VIRAGO' VYAKE GABON Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top