• HABARI MPYA

  Friday, July 08, 2016

  APR MABINGWA TENA LIGI KUU RWANDA KWA MARA YA 16

  APR FC imetwaa taji 16 la Ligi Kuu ya Azam Uganda hiyo ni rekodi, kufuatia waliokuwa wapinzani wao katika mbio za taji, Rayon Sports kufungwa 1-0 Alhamisi jioni na AS Muhanga iliyoshuka daraja Uwanja wa Muhanga.
  Timu hiyo ya Jeshi la nchi hiyo imetetea ubingwa wake kwa kufikisha pointi 67 baada ya kucheza mechi 29 ingawa itahitaji ushindi katika mchezo wake wa Julai 17 dhidi yaAS Kigali ili kuliweka salama taji hilo licha ya ushindi wa kustaajabisha wa Muhanga dhidi ya The Blues wa Kigali.
  APR ilikuwa kileleni kwa Ligi wakiwazidi kwa pointi 10 Rayon Sports wanaofuatia ambao walikuwa wana mechi tatu mkononi ambazo walitakiwa kushinda zote huku wakiiombea timu ya Jeshi ifungwe au kutoa sare na AS Kigali ili wao wawe mabingwa.

  Jenerali Patrick Nyamvumba, Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Rwanda (katikati) akiwa ameshika Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu Rwanda walilotwaa APR msimu uliopita

  APR ilifungwa 1-0 na Rayon Sports Jumatatu katika fainali ya Kombe la Amani, michuano ya Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA) kwa bao la dakika ya mwisho la mshambuliaji wa Mali, Ismaila Diarra.
  Timu zote zitacheza michuano ya Afrika mwakani, APR wakishiriki Ligi ya Mabingwa na Rayon Sports Kombe la Shirikisho.
  APR ndiyo timu yenye mafanikio zaidi katika soka ya Rwanda wakiwa wamechukua mara 16 ubingwa wa Ligi Kuu ya nchi tangu ilipoanzishwa mwaka 1993.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: APR MABINGWA TENA LIGI KUU RWANDA KWA MARA YA 16 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top