• HABARI MPYA

  Sunday, July 03, 2016

  TUYISENGE APIGA ZOTE MBILI GOR MAHIA IKIITANDIKA 2-1 THIKA

  MABINGWA wa Kenya, Gor Mahia wameendeleza wimbi lao la ushindi baaa ya kuilaza mabao 2-1 Thika United leo.
  Shujaa wa Gor Mahia leo alikuwa mwanasoka wa kimataifa wa Rwanda, Jacques Tuyisenge aliyefunga mabao yote mawili kwa K’Ogalo, huo ukiwa ushindi wao wa saba mfululzo katika ligi.
  Tuyisenge alifunga mabao yote mawili kwa kichwa akimalizia krosi za Eric Ouma kumtungua kioa hodari wa Thika, Martin Elungat kipindi cha kwanza.
  Wenyeji walifanikiwa kupata bao la kufutia machozi karibu na mapumziko kupitia kwa Eugene Mukangula.
  Katika mchezo mwingine wa leo, bao la dakika ya 18 la mshambuliaji Noah Wafula limetosha kuwapa Tusker FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Posta Rangers Uwanja wa Machakos.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TUYISENGE APIGA ZOTE MBILI GOR MAHIA IKIITANDIKA 2-1 THIKA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top