• HABARI MPYA

  Saturday, July 09, 2016

  PETR CECH AAMUA KUACHANA NA TIMU YA TAIFA, SASA KAZI ARSENAL TU


  Petr Cech amestaafu soka ya kimataifa baada ya kuichezea Jamhuri ya Czech mechi 121 akimalizia na michuano ya Euro 2016 Ufaransa  PICHA ZAIDI GONGA HAPA 


  REKODI YA PETR CECH JAMHURI YA CZECH

  Mechi: 121
  Alianza: Februari 2002 v Hungary
  Mechi ya mwisho:  Juni 2016 v Uturuki
  Michuano mikubwa: Euro 2004, Kombe la Dunia 2006, Euro 2008, Euro 2012 na Euro 2016
  KIPA wa Arsenal na Jamhuri ya Czech Republic, Petr Cech ametangaza kustaafu ya soka ya kimataifa.
  Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 34 anashikilia rekodi ya kuichezea mechi 121 nchi yake na alicheza mechi zote tatu kikosi cha Pavel Vbra kikitolewa hatua ya makundi Euro 2016 Ufaransa kwa kuambulia pointi moja tu.
  Cech alianza kucheza soka ya kimataifa mwaka 2002 na akaichezea Jamhuri ya Czech katika Euro ya 2004 - ambako walishika nafasi ya tatu - na Kombe la Dunia 2006 kabla ya kurudi kwenye Euro 2008.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PETR CECH AAMUA KUACHANA NA TIMU YA TAIFA, SASA KAZI ARSENAL TU Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top