• HABARI MPYA

  Friday, July 01, 2016

  NEYMAR 'AWAACHA SOLEMBA' MAN UNITED, ASAINI MKATABA MPYA BARCA

  MBRAZIL Neymar amesaini Mkataba mpya wa miaka mitano kuendelea kuichezea Barcelona ya Hispania na sasa atadumu Camp Nou hadi mwaka 2021.
  Ikiwa Neymar mwenye umri wa mika 24 atataka kuwahama vigogo hao wa Hispania atatakiwa kuwalipa Pauni Milioni 167 katika mwaka wa kwanza wa Mkataba wake, Pauni Milioni 185 katika mwaka wa pili na Pauni Milioni 210 katika miaka yote kati ya mitatu iliyobaki.
  Habari hizo zinazima uvumi uliokuwa ukimhusisha Neymar kuhamia Manchester United, wakati Paris Saint-Germain pia ilikuwa inamtaka nyota huyo aliyefunga mabao 31 katika mechi 49 za mashindano yote msimu uliopita. 
  Taarifa katika tovutia ya Barcelona imesomeka: "FC Barcelona na mchezaji Neymar Jr wamesaini Mkataba wa nyongeza na mwanasoka, ambao utamuweka katika klabu kwa miaka mingine mitano hadi Juni 30, 2021. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NEYMAR 'AWAACHA SOLEMBA' MAN UNITED, ASAINI MKATABA MPYA BARCA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top