• HABARI MPYA

    Friday, July 01, 2016

    MANJI: MKATABA WA TBL ULIKUWA HARAMU YANGA

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    MWENYEKITI wa Yanga, Yussuf Manji amesema kwamba alilazimika kuuvunja Mkataba wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kutokana na kwamba ulikuwa haramu.
    Katika taarifa yake kwa vyombo vya Habari leo, Manji amesema kwamba amevunja Mkataba na huo kuingia Mkataba na Kampuni ya International Marketing ili iitafutie klabu wafadhili wengine wa kuziba pengo la TBL kwa ajili ya mishahara ya Juni. 
    "Mkataba wa kampuni ya bia nchini (TBL) na Yanga ulisainiwa miaka mitano iliyopita na mtangulizi wangu.  Huu ulikuwa mkataba haramu, kwani mamlaka ya kutia saini mikataba kwa mujibu wa Katiba ya Yanga yapo kwa wadhamini na hapana kitu kama azimio kutoka  bodi ya wadhamini kuingia katika makubaliano kama haya, au mkataba kusainiwa na wadhamini,"imesema taarifa ya Manji.
    Amesema katika kipindi chake kilichopita alijitahidi kurekebisha tofauti zote zilizokuwepo kwenye Mkataba huo, lakini alishindwa. 
    Yanga waliachana na TBL rasmi Jumanne kwa kuvaa jezi za Quality Group
    "TBL ni mara moja tu imetoa Sh. 20 Millioni kwa ajili ya tamasha la Yanga Day zilizoahidiwa kutolewa kila mwaka, haijailipa klabu fedha ya marekebisho inayofikia Sh. 30 Milioni wala haijatupa basi kwa kiwango sahihi tulichotaka kama ililoahidi katika mkataba.  TBL imejulishwa kuhusu hili lakini haijalishughulikia,"imesema taarifa hiyo.
    Manji amesema International Marketing ni kampuni ambayo alikuwa Mwenyekiti wake na ikakubali ufadhili huo wa mwezi mmoja, jambo ambalo liliifanya Yanga kuvaa jezi za nembo yake Quality Group katika mchezo dhidi ya TP Mazambe.
    "Iwapo wanachama wa Yanga wakihisi nilivunja katiba kwa maslahi yangu binafsi au wakiwa na sehemu nyingine bora zaidi ya kufanya hivyo, walifikishe suala hilo kwenye kamati ya maadili ya klabu kwa ajili ya uamuzi," amesema Manji katika taarifa yake.
    Manji ameongeza kwamba achaguliwa katika mazingira ya amani zaidi miongoni mwa vyama vya soka nchini na ambapo hakuna hata senti moja ilitumika kwa ajili ya kumhonga yeyote.
    "Nilisimama bila kupingwa kugombea nafasi ya Mwenyekiti na nikawaambia wapiga kura wangu waziwazi kwamba: Wakati huu nikiwa Mwenyekiti sitakaa kimya kwa wale watakaojikita katika kuhujumu masuala ya fedha klabuni na wale wanaoamini kwamba TFF iko juu ya sheria zinazohusu masuala ya biashara na haihusiki na Katiba ya Tanzania.  Nawashukuru wapiga kura wangu ambao walinipigia kura kwa asilimia 100 ya ushindi wangu,".
    "Masuala yanayotokea uwanjani au usajili wa wachezaji ni ya soka na kwamba TFF ina mamlaka ya  kuipeleka mbele nchi yetu kwa kufuata miongozo ya FIFA.  Lakini sitavumilia upuuzi wa TFF kutaka kuingilia masuala ya Yanga.  Tunajua FIFA imechafuka kwa rushwa na kusababisha Sepp Blatter kuong’olewa na kukabiliwa na mashitaka: hata hivyo, iwapo tungetumia kauli za TFF, Blatter na Platini wasingefanywa chochote,".
    "Masuala ya fedha ya klabu yetu, yawe kuhusu nembo ya klabu kwenye kituo cha televisheni bila ya kibali cha Yanga si ya kuamuliwa na TFF.  Kilichopo ni kwamba  kitu cha televisheni kinatengeneza fedha kutoka kwa Yanga, TFF inatengeneza fedha kutoka kituo cha televisheni.  Hivyo, iwapo kuna mtu anafikiri sijui sheria za mashindano  bora ya kibiashara na hakimiliki, basi wajue hilo litawagharimu,".
    "Iwapo TFF inataka Mwenyekiti wa Yanga akubaliane na uwongo, basi katika miaka minne ijayo niko tayari kupambana na uovu huo na kusahihisha kila kitu.    Hata hivyo, kwanza kabisa niko tayari  kushirikiana kirafiki  na wakati huohuo kupigania haki za klabu kwani daima nimekuwa mtu mwenye kupigania haki na masuala ya kikanuni ninayoyaamini ni ya kiadilifu,".
    "Yanga ilikuwepo kabla yangu na itakuwapo baada yangu.  Ni wajibu wangu kuiacha Yanga ikiwa klabu bora zaidi kuliko nilivyoikuta na nikiona siwezi tena kutumikia maslahi ya wanachama wake, sitasita kujiuzulu au kuitisha uchaguzi ili kujipanga upya,".
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    1 comments:

    , said... November 12, 2022 at 12:30 PM

    Sikuamini kuwa ningeweza kuungana tena na mpenzi wangu wa zamani, nilipatwa na kiwewe cha kusimama peke yangu bila mwili wa kusimama na kuwa nami, lakini nilipata bahati sana siku moja nilikutana na Dk DAWN, baada ya kumwambia. kuhusu hali yangu alifanya kila liwezekanalo kumuona mpenzi wangu anarudi kwangu, kiukweli baada ya kunifanyia uchawi mpenzi wangu wa zamani alirudi kwangu chini ya masaa 48, mpenzi wangu wa zamani alirudi huku akiniomba kuwa hatoniacha kamwe. tena. Miezi 3 baadaye tulioana na kuoana, ikiwa una hali sawa. Ana nguvu nyingi katika mambo yake;
    * upendo
    inaelezea * inaelezea kivutio
    * kama unataka ex wako nyuma
    *acha talaka
    *kuvunja mawazo
    * huponya viharusi na magonjwa yote
    * uchawi wa kinga
    *Ugumba na matatizo ya ujauzito
    * bahati nasibu
    * bahati nzuri
    Wasiliana na Dk Ediomo kwenye barua pepe yake: dawnacuna314@gmail.com
    Whatsapp:+2349046229159

    Item Reviewed: MANJI: MKATABA WA TBL ULIKUWA HARAMU YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top