• HABARI MPYA

  Friday, July 01, 2016

  MAVUGO: NAKUJA KUSAINI MIAKA MIWILI SIMBA SC

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Burundi, Laudit Mavugo amesema kwamba atawasili nchini wakati wowote kusaini Mkataba wa kujiunga na vigogo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba SC.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE kwa simu leo kutoka Bujumbura, Mavugo amesema kwamba amefikia makubaliano na uongozi wa Simba katika mazungumzo ya awali.
  Mavugo amesema anasubiri kutumiwa tiketi aje Tanzania kwa mazungumzo ya mwisho na kusaini Mkataba.
  “Ninakuja Simba, nadhani mambo yakienda vizuri nitasaini Mkataba wa miaka miwili, tumezungumza vizuri tu na watu wa Simba, tumeelewana,”amesema. 

  Laudit Mavugo amesema kwamba anakuja kusaini Mkataba wa kujiunga na Simba SC

  Simba ilijaribu bila mafanikio kumajili Mavugo msimu uliopita baada ya kushindwa dau kubwa ililotakiwa kutoa ili kumpata.
  Na hiyo ilifuatia klabu mbili za Burundi kupandisha thamani ya mchezaji huyo na kuwa Sh. Milioni 200, badala 110 walizokubaliana awali.
  Aidha, kuibuka pia kwa mzozo mpya kati ya klabu ya Vital’O FC na Solidarity FC, inayodai kumlea Mavugo na kudai ina hakimiliki ya mchezaji huyo nako kuliishitua Simba.
  Vital’O ikaikoroga zaidi Simba SC baada ya kudai kiwepo kipengele cha wao kupata asilimia 50 kama mchezaji huyo atauzwa na Wekundu hao wa Msimbazi kwenda klabu nyingine.   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAVUGO: NAKUJA KUSAINI MIAKA MIWILI SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top