• HABARI MPYA

  Tuesday, July 12, 2016

  MAFARO KUCHEZESHA YANGA NA MEDEAMA JUMAMOSI TAIFA

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  MAREFA wa Misri watachezesha mchezo wa mwisho mzunguko wa kwanza Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika kati ya wenyeji, Yanga SC na Medeama FC ya Ghana Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Taarifa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE jioni ya leo imewataja marefa hao kuwa ni Ibrahim Nour El Din atakayepuliza filimbi akisaidiwa na Ayman Degaish na Samir Gamal Saad.
  Ibrahim Nour El Din ndiye atakayepuliza filimbi katika mchezo kati ya Yanga na Medeama FC Jumamosi

  Mchezo huo utakaoonyeshwa moja kwa moja na Azam TV, unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Yanga nchini kote.
  Na kurushwa moja kwa moja na Azam TV ni faraja kwa wapenzi wa timu hiyo waishio nje ya Jiji hilo ambao wataushuhudia kupitia Televisheni hiyo ya kulipia. 
  Yanga inaendelea na mazoezi Uwanja wa Boko Veterani, Dar es Salaam huku ikiwa imeweka kambi hoteli Ludger Plazza, Kunduchi kujiandaa na mchezo wa tatu wa kundi lake, wakati Medeama inatarajiwa kuwasili kuanzia leo.
  Yanga inahitaji ushindi dhidi ya Medeama baada ya kupoteza mechi zote mbili za mwanzo wakifungwa 1-0 mara zote – na Mo Bejaia nchini Algeria Juni 19 na TP Mazembe ya DRC Dar es Salaam Juni 28.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAFARO KUCHEZESHA YANGA NA MEDEAMA JUMAMOSI TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top