TIMU ya Dodoma Jiji imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya KMC FC katika mchezo Wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Mabao ya Dodoma Jiji yamefungwa na mshambuliaji Faraj Kayanda dakika ya 43 na winga Iddi Bahati Kipagwile dakika ya 77, wakati la KMC limefungwa na mshambuliaji Rashid Mohamed Chambo dakika ya 76.
Kwa ushindi huo, Dodoma Jiji FC inatimiza pointi 17 katika mchezo Wa 14 na kuruka kutoka nafasi ya nane hadi ya sita, wakati KMC inaendelea kushika mkia kwenye ligi ya timu 16 ikibaki na pointi nane za mechi 14 sasa.



.png)
0 comments:
Post a Comment