• HABARI MPYA

  Tuesday, July 12, 2016

  MKATABA MPYA WA AZAM TV, KLABU KUNUFAIKA MARA MBILI YA MSIMU ULIOPITA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAMPUNI ya Azam TV jana imeingia mkataba mpya wa miaka mitano wenye thamani ya Sh. Milioni 23 na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuendelea kurusha moja kwa moja Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ambao ndani yake kuna ongezeko la dau kwa timu zinazoshiriki ligi hiyo.
  Mkurugenzi wa Azam Media, Tido Mhando alimkabidhi Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa mfano wa hundi ya Sh. Bilioni 23 na kusema kwamba msimu mpya utakuwa na mabadiliko makubwa kwenye urushaji wa matangazo ya Ligi Kuu.
  Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa akipokea mfano wa hundi ya Sh. Bilioni 23 kutoka kwa Mkurugenzi wa Azam Media, Tido Mhando (kushoto)
  Mhando alisema katika Mkataba wa awali, kila klabu ilikuwa inapata Sh Milioni 100 kwa msimu, lakini sasa kila klabu itaingiza karibu mara mbili ya fedha hizo.
  “Katika mkataba uliosainiwa leo, klabu itapata Sh milioni 42 kwa mafungu matatu ambayo ni Sh milioni 126. Fungu la mwisho la milioni 42 litatolewa kwa mfumo tofauti ambao utakuwa hivi. Timu inayoshika nafasi ya juu katika msimamo inafaidika kwa kupata zaidi na itakwenda hivyo hadi chini,”alisema Mhando.
  Alisema ligi itakapokwisha, timu zitazokuwa juu katika msimamo zitapata fedha nyingi kuliko za chini, ambazo zitaendelea kusota kwa kupata kiduchu na kwamba lengo kuu ni kuhakikisha kunakuwa na ushindani wa kila kikosi kuona umuhimu wa kukaa juu katika msimamo wa ligi, hali itakayochangia ushindani uwanjani kwa kila timu kutaka kushinda karibu kila mechi ili mwisho wa ligi ifaidike.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MKATABA MPYA WA AZAM TV, KLABU KUNUFAIKA MARA MBILI YA MSIMU ULIOPITA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top