• HABARI MPYA

    Tuesday, July 12, 2016

    YANGA NA MEDEAMA ‘LIVE’ AZAM TV JUMAMOSI

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    MCHEZO wa mwisho wa mzunguko wa kwanza wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika kati ya wenyeji, Yanga SC na Medeama FC ya Ghana utaonyeshwa moja kwa moja na Azam TV.
    Mchezo huo utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Jumamosi, unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Yanga nchini kote na kurushwa moja kwa moja na Azam TV ni faraja kwa wapenzi wa timu hiyo waishio nje ya Jiji hilo. 
    Yanga inaendelea na mazoezi Uwanja wa Boko Veterani, Dar es Salaam huku ikiwa imeweka kambi hoteli Ludger Plazza, Kunduchi kujiandaa na mchezo wa tatu wa kundi lake, wakati Medeama inatarajiwa kuwasili kuanzia leo.
    Yanga inahitaji ushindi dhidi ya Medeama baada ya kupoteza mechi zote mbili za mwanzo wakifungwa 1-0 mara zote – na Mo Bejaia nchini Algeria Juni 19 na TP Mazembe ya DRC Dar es Salaam Juni 28.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA NA MEDEAMA ‘LIVE’ AZAM TV JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top