• HABARI MPYA

  Friday, July 08, 2016

  BEKI LA MEDEAMA FC LATUA AZAM FC KWA MAJARIBIO, CHAMAZI PAFURIKA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BEKI wa Medeama FC ya Ghana, wapinzani wa Yanga SC katika Kundi A Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, Nurdin Yusuf ametua Azam FC kwa majaribio. 
  Beki huyo aliwasili Jumatano na Alhamisi akahudhuria mazoezi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam akiungana na wachezaji wengine, makipa Daniel Yeboah kutoka Ivory Coast na Juan Jesus Gonzalez kutoka Hispania waliokuja kwa majaribio pia.
  Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Alhamisi walianza rasmi mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa 2016-17, chini ya benchi jipya la ufundi linaloongozwa na makocha kutoka Hispania.
  Benchi hilo linaongozwa na Kocha Mkuu Zeben Hernandez, Msaidizi wake Yeray Romero, Kocha Mkuu wa Viungo Jonas Garcia na Msaidizi wake, Pablo Borges na Kocha wa Makipa Jose Garcia.
  Baadhi ya nyota wa Azam FC waliohudhuria mazoezi hayo yaliyoanza saa 3.30 asubuhi ni Nahodha John Bocco ‘Adebayor’ na msaidizi wake Himid Mao ‘Ninja’, wengine ni kipa Aishi Manula, Farid Mussa, Erasto Nyoni, Frank Domayo.
  Wengine walioongeza nguvu ni wachezaji wa kikosi hicho waliokuwa kwa mkopo msimu uliopita, viungo Omary Wayne na Bryson Raphael pamoja na mshambuliaji Kelvin Friday.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BEKI LA MEDEAMA FC LATUA AZAM FC KWA MAJARIBIO, CHAMAZI PAFURIKA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top