• HABARI MPYA

  Wednesday, July 06, 2016

  ALIYETUPIWA VIRAGO AZAM FC AIPA UBINGWA RAYON SPORT RWANDA

  BAO pekee la mshambuliaji wa zamani wa Azam FC ya Tanzania, Ismailia Diarra Jumatatu lilitosha kabisa kuipa Rayon Sports ubingwa wa Kombe la Amani, maarufu kama Peace Cup nchini Rwanda baada ya kwafunga mahasimu, APR 1-0 mjini Kigali.
  Diarra alifunga bao hilo dakika ya mwisho akimalizia mpira uliomshinda kipa wa APR, Olivier Kwizera baada ya shuti la Pierre Kwizera na kuinua shangwe za mashabiki wa ‘The Blues’ ya rwanda Uwanja wa Amahoro.
  Ismaila Diarra (kushoto) amegeuka lulu Rwanda baada ya kufukuzwa kwa fedheha Azam FC

  Ushindi huo unamaliza ukame wa miaka 11 wa Rayon Sport kushindwa kutwaa Kombe la Peace Cup, ambayo ni michuano ya Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA) tangu mwaka 2005.
  Na kwa ushindi huo, Rayon walipata faranga za Rwanda Milioni 8 (sawa na dola za Kimarekani 10, 541) na tiketi ya kuiwakilisha Rwanda kwenye Kombe la Shirikisho Afrika mwakani, wakati APR 'walisunda' faranga Milioni 4 (dola 5, 270).
  Diarra (kushoto) sasa anaibeba Rayon Sport nchini Rwanda


  Diarra alipokuwa Azam FC kabla ya kutupiwa virago baada ya nusu msimu tu

  Wakati huo huo, AS Kigali iliyoifunga Espoir 1-0, bao pekee la Ernest Sugira imeshika nafasi ya tatu ya michuano hiyo.
  Diarra alisajiliwa Azam FC mwaka juzi, lakini akaachwa baada ya nusu msimu akidaiwa kiwango chake ni kidogo ingawa aliacha kumbukumbu nzuri ya kufunga mabao katika msimu ambao timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ALIYETUPIWA VIRAGO AZAM FC AIPA UBINGWA RAYON SPORT RWANDA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top