• HABARI MPYA

    Tuesday, April 14, 2026

    KMC FC YALAZIMISHWA SARE YA KUFUNGANA BAO 1-1 NA PRISONS MWENGE


    TIMU ya KMC imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
    Tanzania Prisons ilitangulia kwa bao la mshambuliaji wake, Jeremiah Juma dakika ya tano, kabla ya kiungo Adam Uledi kuisawazishia KMC dakika ya 38.
    Kwa matokeo hayo, KMC inafikisha pointi tisa, ingawa inaendelea kushika mkia katika ligi ya timu 16 ikizidiwa pointi tano na Tanzania Prisons inayofuatia juu yake, nafasi ya 15 baada ya timu hizo kucheza mechi 19 kila moja.
    Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
    Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KMC FC YALAZIMISHWA SARE YA KUFUNGANA BAO 1-1 NA PRISONS MWENGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top