TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiki hui Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Mabao ya Azam FC yamefungwa na mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Jephte Kitambala Bola dakika ya 48 na winga Iddi Suleiman Ally ‘Nado’ mawili dakika ya 56 na 60.
Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 37, ingawa inabaki nafasi ya tatu, ikizizidi pointi nane zote, JKT Tanzania na Singida Black Stars baada ya timu zote tatu kucheza mechi 19.



.png)
0 comments:
Post a Comment