• HABARI MPYA

  Friday, July 01, 2016

  URENO YATINGA NUSU FAINALI EURO 2016, YAING'OA KWA MATUTA POLAND

  Wachezaji wa Ureno wakishangilia baada ya mwenzao, Ricardo Quaresma kufunga penalti ya mwisho na kuiwezesha timu hiyo kushinda kwa penalti 5-3 mchezo wa Robo Fainali ya Euro 2016 dhidi ya Poland usiku huu Uwanja wa Stade Velodrome mjini Marseille, Ufaransa. Robert Lewandowski alitangulia kuifungia Poland sekunde ya 100, kabla ya Renato Sanches kuisawazishia Ureno dakika ya 33. Wengine waliofunga penalti za Ureno ni Cristiano Ronaldo, Renato Sanches, Joao Moutinho na Luis Nani, wakati za Poland zilifungwa na Robert Lewandowski, Arek Milik na Kamil Glik, huku ya Jakub Blaszczykowski ikichezwa na kipa Rui Patricio. Ureno sasa itacheza na mshindi kati ya Ubelgiji na Wales katika Nusu Fainali Julai 6  PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: URENO YATINGA NUSU FAINALI EURO 2016, YAING'OA KWA MATUTA POLAND Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top