• HABARI MPYA

    Thursday, July 21, 2016

    PLUIJM AONGEZA MIAKA MIWILI KUENDELEA NA KAZI YANGA SC

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    MHOLANZI, Hans van der Pluijm amesaini Mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kufundisha klabu ya Yanga ya Dar es Salaam.
    Pluijm amesaini Mkataba huo jana makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaama baada ya kazi nzuri msimu uliopita, akiipa timu mataji yote matatu ya nyumbani.
    Pluijm aliiwezesha Yanga kuwapiku wapinzani wao wakubwa, Azam FC katika mbio za mataji ya Ngao ya Jamii, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC).

    Pluijm akisaini Mkataba mpya wa kuendelea kufundisha Yanga SC jana

    Na pia akaiwezesha timu hiyo kukata tiketi ya kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuitoa Sagrada Esperanca ya Angola.

    Yanga iliangukia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa na Al Ahly ya Misri katika hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
    Na pamoja na kucheza mechi tatu za Kundi A Kombe la Shirikisho bila ushindi, wakifungwa 1-0 na TP Mazembe, sare ya 1-1 na Medeama zote nyumbani Dar es Salaam na kufungwa 1-0 na MO Bejaia Algeria, lakini Pluijm amepewa Mkataba mpya.  
    Ikumbukwe, Pluijm yupo katika kipindi cha pili kufundisha Yanga baada ya awali kufundisha kwa nusu msimu mwaka 2014, akimpokea Mholanzi mwenzake, Ernir Brandts.
    Alikwenda Al Shoalah FC ya Saudi ya Arabia na nafasi yake ikachukuliwa na Mbrazil, Marcio Maximo ambaye naye alifanya kazi kwa nusu msimu kabla ya Pluijm kurejeshwa Januari mwaka jana. 
    Saudi Arabia ambako alikwenda na aliyekuwa Msaidizi wake, Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa – Pluijm  aliondoka baada ya kutofautiana na uongozi wa timu uliotaka kumsajilia wachezaji asiowataka.
    Franciscus Johannes ‘Hans’ van der Pluijm alizaliwa Januari 3 mwaka 1949 na alianzia kwenye kucheza soka akiwa kipa.
    Enzi zake aliidakia kwa miaka 28 klabu ya FC Den Bosch akicheza mechi 338 ndani ya misimu 18 na alipostaafu baada ya kuumia goti akawa kocha wa timu hiyo.
    Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit akimshuhidia Pluijm anavyotia dole gumba kwenye fomu za Mkataba mpya
    Alianza vyema ukocha akiiwezesha FC Den Bosch kutwaa ubingwa wa Daraja la Kwanza na kupanda Ligi Kuu na ndiye aliyempa nafasi ya kwanza mshambuliaji Ruud van Nistelrooy akiwa kinda wa miaka 17 tu kucheza kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
    Aprili mwaka 1995, alisaini Mkataba wa miaka miwili na SBV Excelsior kabla ya kutimuliwa Januari 1997 na nafasi yake ikachukuliwa na Msaidizi wake, John Metgod. 
    Hiyo ilifuatia timu hiyo ya Rotterdam kushinda mechi mbili tu na sare tatu katika mechi 17 za msimu mzima.
    Baada ya kuboronga Ulaya, ndipo akahamia Afrika mwaka 1999, alipokwenda kufundisha Ashanti Gold SC ya Ghana, akianza na Mkataba wa mwaka mmoja. 
    Ajax ya Uholanzi ikanunua hisa katika klabu hiyo Ijumaa ya Juni 18, mwaka 1999 asilimia 51 naye akatupiwa virago na kuhamia Saint-George SA ya Ethiopia kabla ya mwaka 2010 kujiunga na B-juniors Feyenoord ya Ghana, ambayo ni tawi la timu hiyo ya Rotterdam.
    Mwaka 2012 alijiunga na Berekum Chelsea ambako pia alifukuzwa mwaka jana na kuhamia Medeama ya Ghana pia ambako nako alifukuzwa baada ya mechi saba tu, kufuatia matokeo mabaya mwanzo mwa msimu, akivuna pointi nane kati ya 21.
    Hans van der Pluijm ndiye kocha bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu uliopita 

    MECHI ZOTE ZA PLUIJM YANGA SC
    AWAMU YA KWANZA
    Yanga SC 0-0 KS Flamurtari Vlore (Ziara ya Uturuki)
    Yanga SC 2-2 na Simurq PIK (Ziara ya Uturuki)
    Yanga SC 2-1 Ashanti United (Ligi Kuu Bara)
    Yanga SC 0-0 Coastal Union (Ligi Kuu Bara)
    Yanga SC 1-0 Mbeya City (Ligi Kuu Bara)
    Yanga SC 7-0 Komorozine (Ligi ya Mabingwa)
    Yanga SC 5-2 Komorozine (Ligi ya Mabingwa )
    Yanga SC 7-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu ya Bara)
    Yanga SC 1-0 Al Ahly (Ligi ya Mabingwa)
    Yanga SC 0-1 Al Ahly (Ligi ya Mabingwa. Yanga ilitolewa kwa penalti 4-3)
    Yanga SC 0-0 Mtibwa Sugar  (Ligi Kuu Bara)
    Yanga SC 1-1 Azam FC (Ligi Kuu)
    Yanga SC 2-0 Rhino Rangers (Ligi Kuu)
    Yanga SC 5-0 Prisons (Ligi Kuu)
    Yanga SC 1-2 Mgambo JKT (Ligi Kuu)
    Yanga SC 5-1 JKT Ruvu (Ligi Kuu)
    Yanga SC 2-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu)
    Yanga SC 2-1 JKT Oljoro (Ligi Kuu)
    Yanga SC 1-1 Simba SC (Ligi Kuu)
    AWAMU YA PILI
    Yanga SC 2-2 Azam FC (Ligi Kuu Bara)
    Yanga SC 4-0 Taifa Jang’ombe (Kombe la Mapinduzi, Zanzibar)
    Yanga SC 4-0 Polisi (Kombe la Mapinduzi, Zanzibar )
    Yanga SC 1-0 Shaba (Kombe la Mapinduzi)
    Yanga SC 0-1 JKU (Robo Fainali Kombe la Mapinduzi)
    Yanga SC 0-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu)
    Yanga SC 1-0 Polisi Moro (Ligi Kuu)
    Yanga SC 0-0 Ndanda FC (Ligi Kuu)
    Yanga SC 1-0 Coastal Union (Ligi Kuu)
    Yanga SC 2-0 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu)
    Yanga SC 2-0 BDF XI (Yanga SC 1-2 BDF (Kombe la Shirikisho nyumbani)
    Yanga SC 3-0 Priosns (Ligi Kuu)
    Yanga SC 3-1 Mbeya City (Ligi Kuu)
    Yanga SC 1-2 BDF (Kombe la Shirikisho ugenini)
    Yanga SC 0-1 Simba SC (Ligi Kuu)
    Yanga SC 5-1 Platinum FC (Kombe la Shirikisho)
    Yanga SC 2-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu)
    Yanga SC 2-0 Mgambo JKT (Ligi Kuu)
    Yanga SC 3-1 JKT Ruvu (Ligi Kuu)
    Yanga SC 0-1 FC Platinum (Kombe la Shirikisho Zvashavane)
    Yanga SC 8-0 Coastal Union (Ligi Kuu)
    Yanga SC 3-1 Mbeya City (Ligi Kuu)
    Yanga SC 1-1 Etoile du Sahel (Kombe la Shirikisho)
    Yanga SC 3-2 Stand United (Ligi Kuu)
    Yanga SC 5-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu)
    Yanga SC 4-1 Polisi Moro
    Yanga SC 0-1 Etoile du Sahel (Kombe la Shirikisho)
    Yanga SC 1-2 Azam FC (LIgi Kuu)
    Yanga SC 0-1 Ndanda FC (Ligi Kuu)
    Yanga SC 3-2 Friends Rangers (Kirafiki Karume)
    Yanga SC 0-0 SC  Villa (Kirafiki Taifa)
    Yanga SC 1-0 KMKM (KIrafiki Taifa)
    Yanga SC 3-0 Polisi Kombaini (KIrafiki Taifa)
    Yanga SC 1-2 Gor Mahia (Kagame Taifa)
    Yanga SC 3-0 Telecom (Kagame Taifa)
    Yanga SC 1-0 Khartoum N (Kagame Taifa)
    Yanga SC 0-0 Azam FC pen (3-5 Robo Fainali Kagame Dar)
    Yanga SC 4-1 Kemondo FC (Kirafiki Mbozi. Mbeya)
    Yanga SC 2-0 Prisons (Kirafiki Mbeya)
    Yanga SC 3-2 Mbeya City (Kirafiki Mbeya)
    Yanga SC 0-0 Azam FC (8-7 penalti Ngao ya Jamii)
    Yanga SC 2-0 Coastal Union (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 3-0 Prisons (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 4-1 JKT Ruvu (Ligi Kuu Taifa) 
    Yanga SC 2-0 Simba SC (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 1-1 Azam FC (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga 4-1 Toto Africans (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 2-2 Mwadui FC (Ligi Kuu Shinyanga)
    Yanga SC 2-0 Kagera Sugar (Ligi Kuu Tabora)
    Yanga SC 0-0 Mgambo JKT (Ligi Kuu Mkwakwani)
    Yanga SC 1-0 African Sports (Ligi Kuu Mkwakwani)
    Yanga SC 4-0 Stand United (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 4-2 Friends Rangers (Kirafiki Boko)
    Yanga SC 3-0 Mbeya City (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 3-0 Mafunzo (Kombe la Mapinduzi)
    Yanga SC 1-1 Azam FC (Kombe la Mapinduzi)
    Yanga SC 2-1 Mtibwa Sugar (Kombe la Mapinduzi)
    Yanga SC 1-1 URA (URA ilishinda penalti 4-3 Nusu Fainali Kombe la Mapinduzi)
    Yanga SC 1-0 Ndanda (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 5-0 Majimaji FC (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 3-0 Majimaji FC (Kombe la TFF Taifa)
    Yanga SC 0-2 Coastal Union (Ligi Kuu Mkwakwani)
    Yanga SC 2-2 Prisons (Ligi Kuu Sokoine, Mbeya)
    Yanga SC 4-0 JKT Ruvu (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 1-0 Cercle de Joachim (Ligi ya Mabingwa Mauritius)
    Yanga SC 2-0 Simba SC (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 2-1 JKT Mlale (Kombe la TFF Taifa)
    Yanga SC 2-0 Cercle de Joachim (Ligi ya Mabingwa Taifa)
    Yanga SC 2-2 Azam FC (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 5-0 African Sports (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 2-1 APR (Ligi ya Mabingwa Amahoro, Kigali)
    Yanga SC 1-1 APR (Ligi ya Mabingwa Taifa, Dar)
    Yanga SC 2-1 Ndanda FC (Kombe la TFF Taifa)
    Yanga SC 3-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga 1-1 Al Ahly (Ligi ya Mabingwa, Taifa)
    Yanga SC 1-0 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga 1-2 Al Ahly (Ligi ya Mabingwa, Alexandria)
    Yanga 2-1 Coastal Union (Kombe la TFF, Mkwakwani, mechi ilivunjika dakika ya 110 Yanga ikiwa inaongoza 2-1 baada ya mashabiki wa Coastal kumjeruhi kwa jiwe mshika kibendera namba mbili, Charles Simon wa Dodoma. Siku tatu baadaye, TFF ikaiidhinisha Yanga kucheza fainali)
    Yanga SC 2-1 Mgambo JKT (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 2-1 Toto Africans (Ligi Kuu Kirumba)
    Yanga SC 3-1 Toto Africans (Ligi Kuu Kirumba)
    Yanga SC 2-0 Sagrada Esperanca (Kombe la Shirikisho Afrika Taifa)
    Yanga SC 2-0 Mbeya City (Ligi Kuu Sokoine)
    Yanga SC 2-2 Ndanda FC (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 0-1 Sagrada Esperanca (Kombe la Shirikisho Afrika Angola)
    Yanga 2-2 Majimaji (Ligi Kuu Songea)
    Yanga 3-1 Azam FC (Fainali Kombe la TFF Taifa)
    Yanga 0-1 MO Bejaia (Kundi A Kombe la Shirikisho Bejaia)
    Yanga 0-1 TP Mazembe (Kundi A Kombe la Shirikisho Taifa)
    Yanga 1-1 Medeama (Kundi A Kombe la Shirikisho Taifa)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PLUIJM AONGEZA MIAKA MIWILI KUENDELEA NA KAZI YANGA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top