• HABARI MPYA

  Monday, July 18, 2016

  ODEMWINGIE ATUA HULL CITY KWA MAJARIBIO

  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Nigeria, Peter Odemwingie amejiunga na Hull City kwa majaribio kumshawishi kocha Steve Bruce anayetaka kuimarisha safu yake ya ushambuliaji amsajili kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya England.
  The Tigers wamethibitisha mkongwe huyo wa Nigeria atapewa nafasi katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Mansfield Jumanne usiku.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 ameachwa na Stoke City baada ya kupelekwa kwa mkopo wa muda mfupi Bristol City kumalizia msimu.
  Odemwingie aliumia vibaya goti mwanzoni mwa msimu wa 2014-2015 na pamoja na kurudi uwanjani mwanzoni mwa msimu uliopita, mshambuliaji huyo wa zamani wa West Brom ameshindwa kurudi katika ubora wake.
  Inatarajiwa Odemwingie aliyefunga mabao 37 katika mechi 129 za Ligi Kuu ya England, akiwa na klabu za West Brom, Cardiff na Stoke, atasajiliwa Hull City ili uzoefu wake uisaidie timu ya Bruce kuepuka kushuka daraja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ODEMWINGIE ATUA HULL CITY KWA MAJARIBIO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top