• HABARI MPYA

  Monday, July 11, 2016

  MTIBWA SUGAR YAMSAJILI MANDAWA NA BEKI WA NDANDA, PONERA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MABINGWA wa zamani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Mtibwa Sugar ya Morogoro wamemsajili mshambuliaji wa Mwadui FC ya Shinyanga, Rashid Mandawa (pichani kulia).
  Mratibu wa Mtibwa Sugar, Jamal Bayser ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE jana kwamba mbali na mshambuliaji huyo wa zamani wa Kagera Sugar, pia wamemsajili beki wa kati Cassian Ponera kutoka Ndanda FC ya Mtwara. 
  Bayser pia amesema wamefanikiwa kuwaongezea mikataba wachezaji wao kadhaa wakiwemo kipa Said Mohamed na beki wa kati Salim Mbonde.
  "Usajili unaendelea kwa umakini mkubwa chini ya Mwalimu Salum Mayanga kuziba mapengo hususan kwenye eneo la kiungo ambako tumeondokewa na Mzamiru Yassin, Mohamed Ibrahim na Shiza Kichuya ambao wote wameenda Simba,"amesema Bayser.
  Mabigwa hao wa 1999 na 2000 wa Ligi Kuu, wanatarajiwa kuanza rasmi mazoezi Jumatatu hii kujiandaa na msimu mpya.

  Bayser amesema kambi ya mazoezi itaanzia Dar es Salaam kabla kuhamia makao makuu ya timu, Manungu, Turiani mkoani Morogoro wiki moja baadaye.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAMSAJILI MANDAWA NA BEKI WA NDANDA, PONERA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top