• HABARI MPYA

  Monday, July 18, 2016

  MAZEMBE YATOA SARE 0-0 NA BEJAIA ALGERIA...YANGA SASA WAPUMUA

  Na Mwandishi Wetu, BEJAIA
  TP Mazembe ya DRC imelazimisha sare ya bila kufungana na wenyeji, Mouloudia Olympique Bejaia usiku wa Jumapili Uwanja Unite Maghrebine mjini Bejaia, Algeria katika mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika.
  Matokeo hayo yanazidi kuongeza nafasi ya Mazembe kuingia Nusu Fainali ya michuano hiyo, wakifikisha pointi saba baada ya kucheza mechi tatu, wakati MO Bejaia inafikisha pointi tano baada ya mechi tatu pia.
  Thomas Ulimwengu amecheza leo Mazembe ikitoa sare ya 0-0 nchini Algeria leo
  Medeama ya Ghana inashika nafasi ya tatu katika kundi hilo kwa pointi zake mbili, ikifuatiwa na Yanga ya Tanzania yenye pointi moja baada ya timu zote kucheza mechi tatu pia.
  Matokeo hayo yanamaanisha nafasi ya pili katika Kundi hilo ambayo pia inatoa tiketi ya Nusu Fainali, bado iko wazi kwa timu zote.
  Katika mchezo huo, mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu alianza kabla ya kumpisha Deo Gracia Kanda dakika ya 79.
  Mechi zijazo, Yanga watasafiri hadi Ghana kuifuata Medeama Julai 26, wakati Mazembe wanarejea nyumbani, Lubumbashi kuisubiri MO Bejaia Julai 27.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAZEMBE YATOA SARE 0-0 NA BEJAIA ALGERIA...YANGA SASA WAPUMUA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top