• HABARI MPYA

  Monday, July 11, 2016

  MASSA AONDOKA ULAYA, AREJEA AFRIKA KUSINI NA KUSAINI PRETORIA

  KLABU ya Pretoria University ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini imemsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Geoffrey Massa katika mkataba ulioelelezwa wa muda mrefu.
  Massa, anayejiunga na timu hiyo kutoka, Yenicami Agdelen SK ya Cyprus hii inakuwa mara ya pili k3wake kucheza Afrika Kusini baada ya awali kuchezea Jomo Cosmos mwaka 2009.
  "Kama ilivyokuwa wakati nacheza Afrika Kusini mara ya kwanza, nimefurahi kurejea. Napaswa kujitolea kwa uwezo wangu kuisaidia timu wakati wote, kujituma katika mazoezi na kuelekeza fikra zangu katika kila mchezo"alisena.
  Geoffrey Massa amejiunga na Pretoria University ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini kwa mkataba wa muda mrefu

  Massa anaungana na mshambuliaji wa zamani wa Sofapaka, Obadiah Tarumbwa, Lucky Mathosi, Atusaye Nyondo na Fikru Tefera katika orodha ya washambuliaji wapya wa timu hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MASSA AONDOKA ULAYA, AREJEA AFRIKA KUSINI NA KUSAINI PRETORIA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top