• HABARI MPYA

  Tuesday, July 12, 2016

  BEKI LA GHANA LATUA KWA MKOPO OLYMPIAKOS YA UGIRIKI

  BEKI wa Ghana, Mark Asigba Nyaaba amejiunga na vigogo wa Ugiriki, Olympiakos Piraeus na kuongeza matumaini ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 anakwenda timu hiyo kwa mkopo kutoka Veria FC na atakuwa huko kwa msimu wote wa 2016/17.

  Mark Asigba Nyaaba amejiunga na Olympiakos Piraeus ya Ugiriki kwa mkopo

  Mchezaji huyo msimu uliopita alicheza kwa mkopo Panachaiki ya daraja la chini na kufanikiwa kuanza katika mechi 30 za mashindayo yote.
  Sasa Nyaaba anatakiwa kupambana kwa kuonyesha uwezo wake katika timu hiyo ili apate Mkataba.
  Anakuwa mchezaji wa pili wa Ghana kuchezea Olympiakos baada ya Peter Ofori Quaye kung'ara na wababe hao wa Ugiriki mwanzoni mwa miaka ya 2000.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BEKI LA GHANA LATUA KWA MKOPO OLYMPIAKOS YA UGIRIKI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top