• HABARI MPYA

    Monday, July 11, 2016

    MATHEO AREJEA MAZOEZINI YANGA, TAMBWE AWEKEWA ‘DRIPU’ SITA

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI wa Yanga SC, Mrundi, Amissi Joselyn Tambwe leo amelazimika kuwekewa dripu sita ili kurejesha nguvu mwilini mwake, aweze kuanza mazoezi mapema.
    Yanga inatarajiwa kumenyana na Medeama FC ya Ghana katika mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika Jumamosi na kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm anamuhitaji mfungaji huyo bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara kwa ajili ya mchezo huo.
    Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo kwamba Tambwe alipelekwa hospitali leo kuwekewa dripu ili pate nguvu baada ya kudhoofishwa na Malaria iliyompata wiki iliyopita.
    Amissi Tambwe (kushoto) leo amelazimika kuwekewa dripu sita ili kurejesha nguvu mwilini mwake, aweze kuanza mazoezi mapema Yanga

    Hafidh amesema sasa wanatarajia baada ya mapumziko ya saa 24 tangu leo asubuhi, kesho Tambwe ataanza mazoezi taratibu kujiandaa na mchezo huo.
    Aidha, Hafidh amesema mshambuliaji mwingine, Matheo Anthony ambaye aliumia Jumamosi jioni na kushindwa kumalizia mazoezi, amepata nafuu na leo ameanza mazoezi.
    Tambwe aliukosa mchezo uliopita dhidi ya TP Mazembe kutokana na kuwa anatumikia adhabu ya kadi – na sasa anapambana na Malaria ili acheze mechi ijayo.
    Yanga inaendelea na mazoezi Uwanja wa Boko Veterani, Dar es Salaam huku ikiwa imeweka kambi hoteli Ludger Plazza, Kunduchi kujiandaa na mchezo wa tatu wa kundi lake.
    Tayari Yanga SC itawakosa beki Mwinyi Hajji Mngwali, viungo Deus Kaseke na Geoffrey Mwashiuya katika mchezo huo kutokana na kuwa majeruhi.
    Kaseke aliumia kwenye ajali ya pili, wakati Mngwali na Mwashiuya wote wanasumbuliwa na maumivu ya goti na hawataweza kucheza mchezo huo Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Yanga inahitaji ushindi dhidi ya Medeama baada ya kupoteza mechi zote mbili za mwanzo wakifungwa 1-0 mara zote – na Mo Bejaia nchini Algeria Juni 19 na TP Mazembe ya DRC Dar es Salaam Juni 28.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MATHEO AREJEA MAZOEZINI YANGA, TAMBWE AWEKEWA ‘DRIPU’ SITA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top