• HABARI MPYA

  Monday, May 07, 2018

  REFA MBAYA WA RONALDO APEWA FAINALI LIGI YA MABINGWA

  SHIRIKISHO la Soka Ulaya (UEFA), limemteua Mserbia, Milorad Mazic kuchezesha fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baina ya Liverpool na Real Madrid mjini Kiev, Mei 26, mwaka huu.
  Cristiano Ronaldo anaweza asipende kuungana na refa huyo kutokana na kumbukumbu mbaya za maamuzi ya mwamuzi huyo akiichezea timu yake ya taifa, Ureno katika fainali za Kombe lq Dunia.
  Ronaldoa alimkaripia refa Mazic wakati Ureno ikifungwa mabao 4-0 na Ujerumani mwaka 2014 — mechi ambayo ilishuhudiwa beki wa zamani wa Real, Pepe akitolewa kwa kadi nyekundu, baada ya Mario Gotze kupewa penalti nyepesi kufuatia kukutana na Joao Pereira.

  Cristiano Ronaldo (katikati) akimkaripia refa Milorad Mazic wakati Ureno ikifungwa na Ujerumani mwaka 2014 PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  Mazic aliichezesha Real mwanzoni mwa msimu uliopita katika mechi ya kumuaga Timothee Kolodziejczak wa Sevilla, kabla ya wababe hao wa Bernabeu kutwaa Super Cup ya UEFA kwa ushindi wa 3-2 kwenye muda wa nyongeza. 
  Mwamuzi huyo mwenye umri wa miaka 45 mara ya mwisho kuichezesha Liverpool ilikuwa Machi mwaka 2016, wakati kikosi cha Jurgen Klopp kilipotoa sare ya 1-1 Uwanja wa Old Trafford, na kufuzu dhidi ya Manchester United kwa ushindi wa 3-1 katika hatua ya 16 Bora ya Europa League.
  Mazic alikuwa refa pia katika mchezo pekee wa Sam Allardyce kama kocha wa timu ya taifa ya England, wakati kiungo wa Liverpool, Adam Lallana alipofunga bao pekee la ushindi dakika ya mwisho wakiilaza 1-0 Slovakia, baada ya Martin Skrtel kutolewa kwa kadi nyekundu.
  Msimu huu amechezesha mechi tano za Ligi ya Mabingwa Ulaya ikiwemo moja ya Raundi ya awali. Ametoa kadi 18 za njano kwa wastani wa 3.6 kwa mechi.
  Refa Mholanzi, Bjorn Kuipers atachezesha fainali ya Europa League Mei 16 wakati Atletico Madrid itakapomenyana na Marseille mjini Lyon, Ufaransa.
  Hiyo itakuwa fainali ya pili ya Europa League kwa Kuipers, baada ya kuchezesha ya mwaka 2013 Chelsea ikishinda dhidi ya Benfica. Mholanzi huyo pia alichezesha fainali ya Ligi ya Mabingwa mwaka 2014, wakati Atletico ikifungwa na Real.
  Mazic na Kuipers wote wameteuliwa na FIFA kuchezesha fainali za pili mfululizo za Kombe la Dunia mwezi ujao nchini Urusi.
  Wawili hao, wamechezesha fainali mbili za Kombe la Mabara  — Mazic nchini Urusi mwaka jana na Kuipers nchini Brazil mwaka 2013.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REFA MBAYA WA RONALDO APEWA FAINALI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top