• HABARI MPYA

  Tuesday, May 29, 2018

  MISRI WAMSHITAKI RAMOS FIFA AWALIPE EURO BILIONI

  SAKATA la mshambuliaji Mohamed Salah kuiacha fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mapema baada ya kuumia bega limehamia nchini kwao, Misri.
  Mwanasheria wa Misri amesema kwenye televisheni ya taifa kwamba ameanza harakati na kushitaki kudai Euro Bilioni 1 kwa Sergio Ramos.
  Bassem Wahba aamshitaki Nahodha wa Real Madrid kwa kumuumiza Salah mjini Kiev na maumivu makubwa aliyowasababishia watu wa Misri.

  Mwanasheria wa Misri ameshitaki Sergio Ramos kwa kumuumiza Salah na anataka fidia ya Euro Bilioni 1 

   


  Alisema kwenye chaneli ya Sada El-Balad: "Ramos kwa makusudi alimuumiza Mo Salah na anastahili kuadhibiwa kwa kitendo chake. NImefungua kesi malalamiko FIFA. Nitaomba malipo, ambayo yanaweza kufika Euro Bilioni 1 kwa maumivu na athari ambayo Ramos amempa Salah na watu wa Misri,".
  Baada ya kuumia Jumamosi na kutolewa kipindi cha kwanza tu Liverpool ikichapwa 3-1, Salah sasa anapambana na muda kuhakikisha anakuwa fiti kabla ya Fainali za kwanza za Kombe la Dunia kwa Misri ndani ya miaka 28 mwezi ujao.
  Mafarao wa Misri wanatarajiwa kufungua dimba na Uruguay Juni 15.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MISRI WAMSHITAKI RAMOS FIFA AWALIPE EURO BILIONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top