• HABARI MPYA

  Wednesday, May 30, 2018

  SALAH NJE WIKI TATU MISRI, LIVERPOOL, SASA KOMBE LA DUNIA...

  MSHAMBULIAJI Mohamed Salah anaweza kucheza Fainali za Kombe la Dunia kuanzia hatua ya makundi, baada ya Chama cha Soka Misri (EFA) kusema kwamba maumivu ya bega yatamuweka nje kwa wiki tatu.
  Salah amefanyiwa vipimo na matibabu mjini Valencia, Hispania baada ya kuumia bega katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kufuatia kukabiliana na Nahodha wa Real Madrid, Sergio Ramos. 
  Liverpool wanaamini atakuwa nje kwa kiasi cha wiki tatu, ingawa Msiri wanasema zinaweza kupungua na kubaki hata siku 10 .


  Mohamed Salah anaweza kucheza Fainali za Kombe la Dunia kuanzia hatua ya makundi PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  "Mohamed Salah atakuwa nje kwa kiasi cha wiki mbili au tatu kwa sababu ya maumivu ye bega lake," alisema Abou-Rida kuiambai Radio DRN. 
  "Ni vigumu kwake kucheza mechi dhidi ya Uruguay, lakini tunajaribu kuhakikisha anakuwa fiti kabla ya Kombe la Dunia kuanza. Atakuwa nje kwa muda fulani kwa ajili ya matibabu,".
  Misri ipo Kundi A pamoja na wenyeji, Urusi, Saudi Arabia, na Uruguay. Wataanza Juni 15 kwa kumenyana na Urusi kabla ya kuivaa Saudi Arabia Juni 19 na Uruguay Juni 25.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SALAH NJE WIKI TATU MISRI, LIVERPOOL, SASA KOMBE LA DUNIA... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top