• HABARI MPYA

  Sunday, May 27, 2018

  MISRI YAHAKIKISHIWA NA LIVERPOOL SALAH ATACHEZA KOMBE LA DUNIA

  MISRI bado ina matumaini ya kumumia mshambuliaji wake nyota, Mohamed Salah kwenye fainali za Kombe la Dunia licha ya jana kutoka uwanjania analia baada ya kuumia kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
  Salah alimumia bega baada ya kukutana na beki wa Real Madrid, Sergio Ramos na akashindwa kuendelea na mchezo kipindi cha kwanza Liverpool ikichapwa mabao 3-1. 
  Lakini licha ya kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp kuamini yalikuwa maumivu makali, timu ya taifa ya Misri imesema Salah ameumua kidogo bega na akuwa fti kwa Kombe la Dunia. 
  Daktari wa timu ya taifa ya Misri, Dk Mohammed Abu Alaa ameambiwa na timu ya matabibu wa Liverpool kwamba kufuatia vipimo alivyofanyiwa Salah inaonyesha alipata maumivu kwneye maungio ya bega ambalo lilifungwa ili apate ahueni mapema.
  "Daktari ana matumaini ya Salah kuwa na nafasi ya kujiunga na timu ya taifa kwa ajili ya Kombe la Dunia,"amesema.  

  Mohamed Salah atajiunga na timu ya taifa ya Misri kwa ajili ya Kombe la Dunia PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MISRI YAHAKIKISHIWA NA LIVERPOOL SALAH ATACHEZA KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top