• HABARI MPYA

    Thursday, May 24, 2018

    RWANDA WAIDHAMINI ARSENAL KWA MIAKA MITATU

    KLABU ya Arsenal jana imetangaza udhamini wa miaka mitatu wa Rwanda kujitangaza kwenye mikono ya jezi za Washika Bunduki hao.
    Huo utakuwa mkataba wa kwanza rasmi wa Arsenal kwenye mikono ya jezi, ambako kutaandikwa Tembele Rwanda.
    Mkataba huo ni maalum kuitangaza Rwanda amabyo inaibukia kuwa kituo kikubwa cha utalii, nchi ambayo uchumi wake unakua kwa kasi barani Afrika. 
    Tembele Rwanda itabandikwa kwenye jezi za mikono ya aina yote za Arsenal kuanzia msimu ujao na juzi zilizinduliwa rasmi katika hafla maalum ya wadhamini wao wa jezi, Puma.
    Mkataba huo wa dau zuri utafanya pia mradi wa Tembele Rwanda kuwa washirika wakuu wa klabu hiyo ya Kaskazini mwa London.

    Arsenal imetangaza udhamini wa miaka mitatu na kampeni ya Tembelea Rwanda PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RWANDA WAIDHAMINI ARSENAL KWA MIAKA MITATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top