• HABARI MPYA

  Thursday, May 31, 2018

  SIMBA SC WAPAA KENYA KWENDA KUITAFUTA SAFARI YA GOODISON PARK

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIKOSI cha Simba kimeondoka asubuhi ya leo kwa ndege ya KQ kwenda Kenya tayari kwa michauno ya SportPesa Super Cup inayotarajiwa kuanza Jumampili.
  Simba SC wanatarajiwa kufungua dimba na Kariobangi Sharks Jumapili kabla ya mahasimu wao wa jadi, Yanga kuvaana na Kakamega Homeboys Jumatatu 4, mechi zote zikichezwa Uwanja wa Afraha, Nakuru, Gor Mahia itaanza na JKU Juni 3, wakati Singida United itaanza na AFC Leopards Juni 5. 
  Ikumbukwe bingwa wa michuano hiyo ataondoka kitita cha dola za Kimarekani, 30,000, mshindi wa pili dola 10,000, wa tatu dola 7,500 zitakazoishia Nusu Fainali dola 5,000 na za Robo Fainali dola 2,500.
  Kutoka kulia Mohammed Ibrahim, Haruna Niyonzima na Ally Shomary baada ya kuwasili Nairobi 


  Pamoja na dola 30,000, bingwa wa michuano hiyo kwa mwaka huu atapata fursa ya kwenda kumenyana na klabu ya Everton Uwanja wa Goodison Park mjini Walton, Liverpool nchini England.
  Mwaka jana Gor Mahia ilikuwa bingwa wa kwanza wa michuano hiyo baada ya kuwafunga mahasimu wao, AFC Leopard 2-1 katika fainali kwenye michuano iliyofanyika Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC WAPAA KENYA KWENDA KUITAFUTA SAFARI YA GOODISON PARK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top