• HABARI MPYA

  Thursday, May 31, 2018

  MZIMBABWE WA SINGIDA UNITED TAFADZWA KUTINYU AMFUATA PLUIJM AZAM FC

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  KIUNGO Mzimbabwe, Tafadzwa Kutinyu amejiunga na klabu ya Azam FC kutoka Singida United, akimfuata kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm.
  Azam FC tayari imemtangaza Pluijm kuwa kocha wake mpya, akichukua nafasi ya Mromania, Aristica Cioaba aliyeondolewa baada ya matokeo mabaya msimju huu. 
  Pluijm ataiongoza Singida United kwa mara ya mwisho Jumamosi katika fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Mtibwa Sugar akijaribu kuiachia japo taji moja.


  Tafadzwa Kutinyu (kushoto) anamfuata Hans van der Pluijm klabu ya Azam FC  Kutinyu mwenye umri wa miaka 23, alijiunga na Singida United msimu huu akitokea Chicken Inn ya kwao, Zimbababwe sawa na kocha Pluijm aliyeanza kazi timu hiyo Agosti mwaka jana baada ya kuondolewa Yanga.
  Tayari Azam FC imemsajili Mzimbabwe mwingine, mshambuliaji Donald Ngoma kutoka Yanga SC ya Dar es Salaam, ambaye inaaminika pia ni ushawishi wa Pluijm.
  Pluijm alikuja Tanzania mwaka 2014 na kujiunga na Yanga SC alikofanya kazi kwa msimu mmoja kabla ya kwenda Al Shoalah FC ya Saudi Arabia na kurejea Jangwani mwaka 2015 akafanya kazi Novemba 2016 alipohamia Singida United.
  Cioaba alijiunga na Azam FC Januari mwaka jana akichukua nafasi ya makocha Waspaniola, chini ya Zeben Hernandez Rodriguez na ameshinda taji moja moja tu, Kombe la Mapinduzi Januari mwaka huu.
  Katika hatua nyingine, klabu ya Azam FC imebadilisha muundo wake wa uendeshaji na kuanzia msimu ujao itakuwa kampuni.
  Hayo yamesema na mmoja wa Wakurugenzi wa Azam FC, Nassor Idrisa 'Father' katika mahojiano maalum na Azam TV Jumatano.
     
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MZIMBABWE WA SINGIDA UNITED TAFADZWA KUTINYU AMFUATA PLUIJM AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top