• HABARI MPYA

  Sunday, May 27, 2018

  NI REAL MADRID MABINGWA TENA ULAYA, WAIPIGA 3-1 LIVERPOOL KIEV, KIPA...

  TIMU ya Real Madrid imefanikiwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya tatu mfululizo baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Liverpool usiku wa Jumamosi Uwanja wa Olimpiki mjini Kiev, Ukraine. 
  Hilo linakuwa taji la 13 la rekodi la michuano hiyo Kwa Real Madrid, baada ya awali kushinda katika miaka ya 1956, 1957, 1958, 1959, 1960, 1966, 1998, 2000, 2002, 2014, 2016 na 2017; na kufungwa katika fainali za 1962, 1964 na 1981. 
  Liverpool wamecheza fainali ya nane leo, na ya kwanza tangu mwaka 2007, ambayo walishinda kwa jumla ya mabao 7–6 dhidi ya Roma ya Italia wakiwa na rekodi ya kushinda taji hilo mara tano katika miaka ya 1977, 1978, 1981, 1984 na 2005 na leo wamefungwa kwa mara ua tatu kwenye fainali baaada ya mwaka 1985 na 2007. 

  Real Madrid wakishangilia na taji lao la 13 la Ligi ya Mabingwa baada ya kukabidhiwa usiku wa Jumamosi  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Liverpool ilipata pigo mapema tu katika mchezo wa leo, baada ya mshambuliaji wake nyota, Mmisri Mohammed Salah kutolewa nje dakika ya 30 kufuatia kuumia baada ya kugongana na beki na Nahodha wa Real Madrid, Sergio Ramos. 
  Kipa Karius akawazawadia bao la kuongoza Real Madrid baada ya kupiga mpira bila uangalifu mbele ya Karim Benzema ambao ulimgonga na kuingia nyavuni dakika ya 51. 
  Mshambuliaji Msenegali, Sadio Mane akaisawazishia Liverpool dakika nne baadaye, kabla ya Gareth Bale kutokea benchi na kufunga mabao mawili dakika za 64 na 83. 
  Karius aliwasili Liverpool akitokea Mainz mwaka 2016 na alikuwa na mwanzo mgumu kabla ya kuzinduka na kuwa kipa chaguo la kwanza mbele ya kocha Jurgen Klopp akimpindua kipa Simon Mignolet. Lakini makosa ya leo ya Karius hayatasahaulika milele. 
  Kikosi  cha Real Madrid leo kilikuwa; Navas, Carvajal/Nacho, Varane, Sergio Ramos, Marcelo, Modric, Casemiro, Kroos, Isco/Bal, Benzema/Asensio nA Ronaldo
  Liverpool starting XI: Karius, Alexander-Arnold, Lovren, Van Dijk, Robertson, Milner/Can, Henderson, Wijnaldum, Salah/Lallana, Firmino ma Mane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI REAL MADRID MABINGWA TENA ULAYA, WAIPIGA 3-1 LIVERPOOL KIEV, KIPA... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top