• HABARI MPYA

  Wednesday, May 23, 2018

  RAIS WA GHANA AAMURU MWENYEKITI WA FA AKAMATWE

  RAIS wa Ghana, Akufo-Addo ameamuru Mwenyekiti wa Chama Soka Ghana (GFA), Kwesi Nyantekyi akamatwe kwa tuhuma za ufisadi.
  Nyantekyi, ambaye pia ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad anakabiliwa na tuhuma nzito za ufisadi.
  Hiyo ni baada ya makala moja ya uchunguzi kumhusisha Kwasi Nyantekyi na vitendo vya ulaghai.
  Uchunguzi huu uliofanywa na mwandishi wa habari maarufu nchini humo, Anas Aremeyaw Anas uliwasilishwa kwa Rais, aliyechukua hatua hiyo.

  Uchunguzi huu pia unadaiwa kufichua vitendo vya ufisadi miongoni mwa maafisa wengine wa GFA na video hiyo inatarajiwa kuonyeswa hadharani Juni 6, mwaka huu.
  Kwesi Nyantenkyi amekuwa rais wa GFA tangu mwaka 2005 na hadi sasa hajatoa tamko lolote juu ya madai hayo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAIS WA GHANA AAMURU MWENYEKITI WA FA AKAMATWE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top