• HABARI MPYA

  Monday, May 28, 2018

  RONALDO AONYESHA DALILI ATABAKI REAL MADRID, LAKINI...

  MWANASOKA bora wa dunia, Cristiano Ronaldo ameonyesha dalili kwamba atabaki Real Madrid, licha ya kuibua shaka juu ya mustakabali wake baada ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. 
  Wakati wa sherehe za ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Liverpool, Ronaldo aliwaambia mashabiki: 'Tutaonana mwaka mwingine.'
  Alipata mapokezi ya kishujaa huku mashabiki wakitaja jina lake na mshambuliaji huyo akasema: “Najisikia faraja kuchezea klabu kubwa duniani. Niko saw asana hapa. Na kwa wachezaji wale ni vigumu kutoshinda.' 

  Cristiano Ronaldo ameonyesha dalili kwamba atabaki Real Madrid  PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  Baada ya filimbi ya mwisho mjini Kiev usiku wa Jumamosi, Ronaldo alisema; “Siku zijazo kutakuwa na majibu juu ya mustakabali wangu. Imekuwa nzuri sana kuchezea Real Madrid,”.
  Mreno huyo baadaye akasema: “Nimeshinda mataji matano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na tuzo tano za Ballon d'Ors. Tayari nimeweka historia, lakini sasa hata zaidi. Sijabadilika kwa sababu ninajua ninachoipa klabu. Sitaki kuufuta wakati huu wa kipekee, na wenzangu ambao ni mabingwa.  Siwezi kuhakikisha kitu chochote. Siwezi kuficha, katika siku chache zijazo nitazungumza... Maisha si kuhusu utukufu,”.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONALDO AONYESHA DALILI ATABAKI REAL MADRID, LAKINI... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top