• HABARI MPYA

  Thursday, May 24, 2018

  WINGA MWENYE KASI SIMON HAPPYGOD MSUVA AKUBALI KUJIUNGA NA TIMU YA MBWANA ALLY SAMATTA

  Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM
  WINGA wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Simon Happygod Msuva amekubali kuchezea kikosi cha Marafiki wa Mbwana Ally Samatta katika mechi maalum ya hisani dhidi ya Timu ya mwanamuziki Ali Kiba na rafiki zake kuhamasisha uchangiaji wa vifaa na miundombinu mashuleni Juni 9, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo kwa simu kutoka Morocco, winga huyo mwenye kasi Msuva amesema kwamba anaunga mkono kampeni hiyo na atakuwepo Juni 9 kucheza mechi hiyo maalum ya Hisani. “Elimu Bora ni mimi na wewe, tukishirikiana tunaweza kusaidia watoto wetu kufikia malengo,”amesema winga huyo wa zamani wa Yanga.
  Simon Msuva amekubali kuchezea timu ya Mbwana Samatta Juni 9 Uwanja wa Taifa 

  Mratibu wa mechi hiyo, Daniel Cleverest amesema kwamba maandalizi yanaendelea vizuri na mgeni rasmi siku hiyo anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison George Mwakyembe.
  Cleverest amesema kwamba kwa sasa wapo kwenye mazungumzo na kampuni za Azam TC, benki ya DTB, Bin Slum, Tyres Limited na Speshoz ili wawe wadhamini wa mechi hiyo.
  “Bado tupo katika hatua za mwisho na kupangilia mambo, tunatarajia mapema wiki ijayo tutatoa utaratibu na ratiba nzima ya shughuli,”amesema Cleverest.  
  Samatta anayechezea KRC Genk ya Ubeligiji ambaye ni mchezaji wa zamani wa Simba SC ya Dar es Salaam, pia ni Nahodha wa Taifa Stars.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WINGA MWENYE KASI SIMON HAPPYGOD MSUVA AKUBALI KUJIUNGA NA TIMU YA MBWANA ALLY SAMATTA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top