• HABARI MPYA

    Wednesday, May 23, 2018

    ABRAMOVICH SASA ATAKIWA KUTHIBITISHA UHALALI WA UTAJIRI WAKE

    BILIONEA Roman Abramovich atatakiwa kuthibitisha namna alivyopata utajiri wake ili aweze kupatiwa kupatiwa visa ya kuingia tena Uingereza.
    Hatua huyo inafuatia Serikali kuanzisha vita maalum ya kuchunguza namna watu wanavyitajirika na mfanyabiashara huyo wa Urusi, mmiliki wa klabu ya Chelsea FC amefungiwa rasmi kuingia Uingereza hadi hapo atakapoonyesha fedha zake ni safiu.
    Matajiri wengine wakubwa waliopo Uingereza pia wanachunguzwa juu ya namna walivyotajirika na pia wanavyoutumia utajiri wao.

    Roman Abramovich (kushoto) katika picha ya pamoja na Rais Vladimir Putin mwka 2016 PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    Hiyo inafuatia kuibuka kwa mtafaruku baina na nchi hizo mbili, baada ya Uingereza kudai Urusi ilitupa watu wa kwenda kumuwekea sumu jasusi Sergei Skripal na na binti yake mjini Salisbury.
    Serikali ya Uingereza imeilaumu Urusi na Waziri Mkuu, Theresa May amesema tukio hilo ni kama 'kudharauliwa' na akafukuza wanadiplomasia kadhaa wa Kirusi nchini humo.
    Abramovich, ambaye yuko nje ya Uingereza na alikosa fainali ya Kombe la FA, timu yake, Chelsea ikishinda 1-0 dhidi ya Manchester United Jumamosi, anachukuliwa kama muombaji mpya wa visa ya kuingia nchini humo.
    Tayari Rais wa Urusi, Vladimir Putin ambaye ni swahiba wa Abramovich amekwishalalamikia namna Uingereza inavyomfanyia mfanyabiashara huyo, kwamba haimtendei haki.
    Abramovich aliinunua Chelsea mwaka 2003 kwa Pauni Milioni 60.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ABRAMOVICH SASA ATAKIWA KUTHIBITISHA UHALALI WA UTAJIRI WAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top