• HABARI MPYA

  Tuesday, May 29, 2018

  SALAH APELEKWA HISPANIA KWA MATIBABU ZAIDI

  MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Mohamed Salah atasafirishwa kwenda Hispania kesho kwa matibabu ya bega lake, Shirikisho la Soka Misri limesema.
  Mfungaji huyo bora wa Wekundu hao wa Anfield kwa mabao yake 44 alilazimika kutoka uwanjani kipindi cha kwanza Jumamosi kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakifungwa 3-1 na Real Madrid baada ya kuumia bega kufuatia kukabiliana na Sergio Ramos.
  Salah alitweet jana kwamba bado anaamini atakuwepo kwenye kikosi cha Misri kwenye Kombe la Dunia nchini Urusi na Jumatatu jioni ilithibitishwa atakwenda Hispania.

  Mohamed Salah atasafirishwa Hispania kwa matibabu ya bega lake kesho PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Shirikisho la Soka Misri limesema Salah alianza programu ya matibabu Jumapili na mambo yalikwenda vizuri kiasi cha kufufua matumaini ya kuwepo kwenye timu.
  Ataendelea na matibabu Hispania ambako ataongozana na Rais wa Shirikisho la Soka la Misri, Daktari wa timu ya taifa na matabibu wa Liverpool.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SALAH APELEKWA HISPANIA KWA MATIBABU ZAIDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top