• HABARI MPYA

  Sunday, May 27, 2018

  LIVERPOOL WAREJEA NYUMBANI KINYONGE BAADA YA KIPIGO CHA JANA

  KIKOSI cha Jurgen Klopp kimerejea nyumbani baada ya kuchapwa mabao 3-1 na Real Madrid usiku wa jana katika fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya.
  Kikosi hicho kilitua Uwanja wa Ndege wa John Lennon Jumapili asubuhi saa kadhaa baada ya fainali hiyo Uwanja wa Olimpiki mjini Kiev.
  Kocha Klopp alionekana mwenye huzuni wakati wanawasili kufuatia kipigo hicho na kipa Loris Karius, ambaye makosa yake mawili yaliwapa mabao mepesi mawili Madrid jana alionekana mnyonge wakati timu inawasili. 
  Mjerumani huyo aliteremka kwenye ndege maalum binafsi ya Liverpool sambamba na Joel Matip na Emre Can akiendelea kujutia makosa yake mjini Kiev.
  Wachezaji wa Liverpool wakiwemo Loris Karius (wa pili kushoto) wakiteremka kwenye ndege Uwanja wa John Lennon PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  Karius aliwazawadia bao la kuongoza Real Madrid baada ya kupiga mpira bila uangalifu mbele ya Karim Benzema aliyeuzuia na kuingia nyavuni dakika ya 51 na akaruhusu bao la tatu baada ya shuti la mbali la Gareth Bale. 
  Mshambuliaji Msenegali, Sadio Mane akaisawazishia Liverpool dakika nne baadaye, kabla ya Bale kutokea benchi na kufunga mabao mawili dakika za 64 na 83. 
  Karius aliyewasili Liverpool akitokea Mainz ya kwao, Ujerumani mwaka 2016 na alikuwa na mwanzo mgumu kabla ya kuzinduka na kuwa kipa chaguo la kwanza mbele ya kocha Jurgen Klopp akimpindua kipa Simon Mignolet. 
  Liverpool ilipata pigo mapema tu katika mchezo wa leo, baada ya mshambuliaji wake nyota, Mmisri Mohammed Salah kutolewa nje dakika ya 30 kufuatia kuumia baada ya kugongana na beki na Nahodha wa Real Madrid, Sergio Ramos. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL WAREJEA NYUMBANI KINYONGE BAADA YA KIPIGO CHA JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top