• HABARI MPYA

  Tuesday, May 22, 2018

  SAMATTA KUCHEZA MECHI YA HISANI DAR JUNI 9 DHIDI YA ALI KIBA NA RAFIKI ZAKE UWANJA WA TAIFA

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  NAHODHA wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Ally Samatta anatarajiwa kucheza mechi maalum ya hisani kuhamasisha uchangiaji wa vifaa na miundombinu mashuleni Juni 9, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo kwa simu kutoka Genk, Ubelgiji, Samatta amesema kwamba hiuyo itakuwa ni baina yeye na rafiki zake dhidi ya mwanamuziki Ali Kiba na rafiki zake.  
  “Ni mechi ya hisani ya Samatta 11 na Ali Kiba 11, nitachagua rafiki zangu na Ali atachagua rafiki zake. Ni mechi ya Hisani kama nyingine nyingi ambazo zimekuwa zikifanywa na wachezaji wakubwa. Nataka nifanye moja lakini itakuwa na ladha tofauti, kwani timu pinzani itakuwa ya Ali Kiba,”amesema Samatta leo. 

  Mbwana Samatta anatarajiwa kucheza mechi ya hisani Juni 9 Uwanja wa Taifa dhidi ya timu ya Ali Kiba

  Kwa upande Ali Kiba amesema kwamba amefurahi sana urafiki wake na Samatta kuzalisha kitu hicho kizuri na amewaomba wapenzi na mashabiki wake kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Taifa Juni 9 kwenye mchezo huo wa Hisani.
  Naye Mratibu wa mechi hiyo, Daniel Cleverest amesema kwamba maandalizi yanaendelea vizuri na mgeni rasmi siku hiyo anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison George Mwakyembe.
  Cleverest amesema kwamba kwa sasa wapo kwenye mazungumzo na kampuni za Azam TV, benki ya DTB, Bin Slum Tyres Limited na Speshoz ili wawe wadhamini wa mechi hiyo.
  “Bado tupo katika hatua za mwisho na kupangilia mambo, tunatarajia mapema wiki ijayo tutatoa utaratibu na ratiba nzima ya shughuli,”amesema Cleverest.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA KUCHEZA MECHI YA HISANI DAR JUNI 9 DHIDI YA ALI KIBA NA RAFIKI ZAKE UWANJA WA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top