• HABARI MPYA

  Wednesday, May 30, 2018

  SINGIDA UNITED WAWAAMBIA MTIBWA SUGAR; “MNAKUJA KUTALII TU ARUSHA, MABINGWA NI SISI”

  Na Sada Salmin, ARUSHA
  UONGOZI wa Singida United umetamba wao ndiyo mabingwa wapya wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) – kwani wa uhakika wa kuwafunga wapinzani wao, Mtibwa Sugar Jumamosi.
  Singida United na Mtibwa Sugar watakutana katika fainali ya tatu ya Kombe la TFF tangu kurejea kwa michauno huyo mwaka juzi – mchezo ambao utafanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.
  Hiyo ni baada ya safari iliyoviangushia njiani vingunge, Azam, Simba waliokuwa mabingwa watetezi na Yanga na washindi wa mwaka juzi.

  Na kuelekea mchezo huo, Mkurugenzi wa Singida United, Sanga Festo amesema kwamba wako imara na tayri kabisa kwa ajili ya kuweka historia mpya katika soka ya Tanzania.
  “Tuko imara na tuko tayari kabisa kuweka historia mpya katika soka ya Tanzaia kwa kubeba Kombe hili. Tunajua utakuwa mchezo mgumu, lakini tumejipanga vizuri kushinda,”alisema Sanga akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online jana.
  Sanga amesema hali ya kambi ni nzuri na maandalizi ya mwisho mwisho yanaendelea vizuri kuelekea fainali ya ASFC inayitarajiwa kuwa kali na ya kusisimua.
  Wakati Singida United tayari wapo Arusha tangu jana, Mtibwa Sugar wanatarajiwa kuwasili leo mjini humo, nao wakitamba wanakwenda kuchukua Kombe.
  Kwa msimu huu katika mechi mbili zilizozikutanisha timu hizo kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, mechi ya kwanza iliisha kwa sare ya 0-0 Jumapili ya Oktoba 29, mwaka jana Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro na marudiano Ijumaa ya Aprili 6, mwaka huu Mtibwa Sugar ilishinda 3-0 Uwanja wa Namfua mjini Singida.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA UNITED WAWAAMBIA MTIBWA SUGAR; “MNAKUJA KUTALII TU ARUSHA, MABINGWA NI SISI” Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top