• HABARI MPYA

  Thursday, May 31, 2018

  SINGIDA UNITED YASHUSHA MUIVORY COAST NA MBRAZIL, YAKUBALI KUMUUZA KUTINYU AZAM FC

  Na Mwandishi Wetu, ARUSHA
  KLABU ya Singida United leo imesajili wachezaji watatu wapya kuelekea msimu ujao, wakiwemo Muivory Coast kiungo Amara Diaby na Mbrazil mshambuliaji Felipe Oliveira. 
  Pamoja na wageni hao wawili, ambao kila mmoja amesaini mkataba wa miaka miwili, Mkurugenzi wa Singida United, Sanga Festo amesema kwamba klabu pia imemsajili mshambuliaji chipukizi, Tibar John aliyesaini miaka mitatu kutoka Ndanda FC ambaye alikuwa anawaniwa na Yanga SC.
  Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Arusha, Sanga Festo alisema kwamba wachezaji hao wamesaini mikataba na wanajiunga na timu mara moja kwa maandalizi ya msimu mpya.
  Mkurugenzi wa Singida United, Sanga Festo (kulia) akimkabidhi jezi Muivory Coast Amara Diaby leo
  Mshambuliaji Mbrazil Felipe Oliveira akiwa na jezi ya Singida United baada ya kusaini 
  Sanga Festo akimkabidhi mshambuliaji chipukizi, Tibar John jezi ya Singida United 

  Aidha, katika mkutano huo wachezaji na watumishi wa klabu ya Singida United FC kila mmoja amepewa mifuko 50 ya saruji kama zawadi baada ya kumaliza msimu vizuri, timu ikiingia fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports federation Cup (ASFC).
  Sanga pia alisema kwamba mchezaji wao, wamepokea ofa kutoka Azam FC wakimtaka mchezaji wao, kiungo Mzimbabwe Tafadzwa Kutinyu. “Hatuna tatizo na Azam FC, tutakaa chini tuipitia ofa yao na kuwapa majibu”amesema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA UNITED YASHUSHA MUIVORY COAST NA MBRAZIL, YAKUBALI KUMUUZA KUTINYU AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top