• HABARI MPYA

  Friday, May 25, 2018

  RONALDO AKATAA KUFANANISHWA NA SALAH

  MWANASOKA bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo amesema yeye yu tofauti kabisa na kila mchezaji mwingine wa soka – akikataa kufananishwa na mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah. 
  Pamoja na kwamba wote wawili wanapewa nafasi ya kushinda Ballon d'Or ya 2018, lakini Mreno huyo amesema kwamba yeye ni mrefu, Salah ni mfupi mno na yeye anatumia mguu wa kulia, wakati Mmisri huyo anatumia mguu wa kushoto.
  Ronaldo amekiri Salah amekuwa na msimu mzuri Liverpool, lakini kuhusu fainali ya kesho vyema tukasubiri tuone.

  Cristiano Ronaldo amesema yuko tofauti kabisa na Mohamed Salah na kila mchezaji mwingine PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  “Anatumia mguu wa kushoto, natumia mguu wa kulia, mimi ni mrefu, yeye ni mfupi mno. Natumia kichwa pia, unajua – tuko tofauti kabisa. Lakini napaswa kusema amekuwa na msimu mzuri, lakini Jumamosi acha tuone,”amesema Ronaldo.
  Majigambo haya yanakuja siku moja tu kabla ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baina ya timu zao mjini Kiev leo. 
  Wakati Salah atakuwa anapigania taji hilo kubwa Ulaya kwa mara ya kwanza, Ronaldo atakuwa anawania taji la sita, baada ya mara moja kushinda na Man United na mara nne na klabu yake ya sasa, Real Madrid.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONALDO AKATAA KUFANANISHWA NA SALAH Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top