• HABARI MPYA

  Tuesday, May 22, 2018

  SIMBA SC: HATUNA HURUMA NA MAJI MAJI, TUTAWAPIAGA NA WASHUKE SALAMA

  Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Simba SC imesema kwamba haitawahurumia Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara  Jumatatu ijayo Uwanja wa Maji Maji mjini Songea.
  Simba SC tayari mabingwa wa Ligi Kuu kwa pointi zao 68 baada ya kucheza mechi 29, wakishinda 20, sare nane na kufungwa moja, wakati Maji Maji inapigana vita ya kuepuka kushuka daraja.
  Lakini pamoja na hayo, Msemaji wa klabu ya Simba, Hajji Sunday Manara amesema kwamba hawataihurumia Maji Maji, bali wataifunga huko huko ishuke Daraja. 
  Manara amesema kwamba dhamira ya Simba SC ilikuwa kumaliza Ligi Kuu bila kupoteza mchezo, lakini bahati mbaya wamefungwa na Kagera Sugar Jumamosi – hivyo hawataki kupoteza mechi nyingine.

  Hajji Manara amesema kwamba hawatakuwa na huruma na Maji Maji Jumatatu mjini Songea

  “Tumefanikiwa kufikia kutwaa ubingwa bila kupoteza mechi, lakini tumeshindwa kumaliza Ligi Kuu bila kufungwa, sasa tunataka tumalize Ligi Kuu kwa rekodi ya kupoteza mechi moja tu,”amesema Manara.
  Kikosi cha Simba SC kinatarajiwa kuondoka Dar es Salaam Jumamosi kwa basi lake kwenda Songea kwa ajili ya mchezo huo wa mwisho wa Ligi Kuu kukamilisha msimu wa 2017-2018.
  Maji Maji inashika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi Kuu wakiwa na pointi 24 baada ya kucheza mechi 29, mbele ya Ndanda FC iliyo nafasi ya 15 kwa pointi zake 23 za mechi 28 na Njombe Mji FC wenye pointi 22 za mechi 29 pia.    
  Timu mbili zitashuka wiki ijayo na tayari African Lyon, Alliance Schools, Biashara United, Coastal Union, JKT Tanzania na KMC zimepanda ili kuwa na Ligi Kuu ya timu 20 msimu ujao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC: HATUNA HURUMA NA MAJI MAJI, TUTAWAPIAGA NA WASHUKE SALAMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top