• HABARI MPYA

  Tuesday, May 29, 2018

  MTIBWA SUGAR YAIENDEA SINGIDA UNITED NA KIKOSI KAMILI HADI TIMU YA VIJANA WOTE

  Na Mwandishi Wetu, MOROGORO
  KIKOSI cha Mtibwa Sugar kinaondoka kesho Alfajiri Manungu, Turiani mkoani Morogoro kwenda Arusha tayari kwa fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Singida United.
  Mtibwa Sugar na Singida United zinatarajiwa kukutana Juni 2, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha katika fainali ya ASFC.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo, Katibu Mipango wa Mtibwa Sugar, Abubakar Swabur amesema kwamba wataondoka na kikosi kamili cha wachezaji 28 pamoja na wengine 30 wa timu ya vijana kwenda Arusha.
  Swabur amesema kwamba kwa ujumla maandalizi yamekuwa mazuri mno kuelekea fainali hiyo na wachezaji wote wa Mtibwa Sugar wapo fiti hakuna mgonjwa wala majeruhi.
  Swabur amesema kwamba lengo la Mtibwa Sugar ni kutwaa ubingwa wa michuano hiyo ili kurejesha heshima yao kwenye soka ya Tanzania.
  Pamoja na hayo, Swabur amesema siku hiyo watazindua jezi zao maalum za kuwauzia mashabiki siku hiyo ambao pia zitakuwa zinatumika kwenye Komb la TFF kila mwaka.
  Swabur ameendelea kupuuzia kwamba hata wakitaa Kombe la ASFC hawatashiriki micnuano ya Kombe la Shirikisho Afrka kuwa watakuwa wanaendekea kushikilia adhabu ya kufungiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
  Swabur ameema kwamba walimaliza adhabu yao ya kufungiwa miaka mitatu mwaka 2007 na walilipa faini kupitia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kwa sasa wako huru kucheza michuano ya Afrika tangu mwaka 2008.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAIENDEA SINGIDA UNITED NA KIKOSI KAMILI HADI TIMU YA VIJANA WOTE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top