• HABARI MPYA

  Wednesday, May 23, 2018

  NDANDA FC YAIBAMIZA MWADUI 3-0 NA KUISHUSHA NJOMBE MJI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Ndanda FC imepata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mwadui FC jioni ya leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
  Shukrani kwa wafungaji wa mabao hayo leo ambayo yote yalipatikana kipindi cha kwanza, Jacob Massawe dakika ya tatu, Mrisho Ngassa dakika ya tano na Tibar John dakika ya 40.
  Na kwa ushindi huo, Ndanda FC inafikisha pointi 26 baada ya kucheza mechi 29, ingawa inabaki nafasi ya 14 nyuma ya Mbao FC yenye pointi 30 za mechi 29 pia – na mbele ya Maji Maji FC yenye pointi 24 za mechi 29 na Njombe Mji FC yenye pointi 22 za mechi 29, ambayo tayari imekwishashuka Daraja.

  Ligi Kuu itaendelea Ijumaa kwa mchezo mmoja tu, Yanga SC wakimenyana na Ruvu Shooting Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam kabla ya msimu wa 2017-2018 kuhitimishwa Jumatatu kwa timu zote 16 kuteremka uwanjani.
  Timu mbili zitateremka Jumatatu kuzipisha African Lyon, JKT Tanzania, KMC za Dar es Salaam, Alliance Schools ya Mwanza, Biashara United ya Mara na Coastal Union ya Tanga zilizopanda ili kupata timu 20 kuanzia msimu ujao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NDANDA FC YAIBAMIZA MWADUI 3-0 NA KUISHUSHA NJOMBE MJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top